STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 21, 2013

Real Madrid yathibitisha kuacha na Mourinho

 
Kocha Jose Mourinho

KLABU ya Real Madrid imethibitisha kuwa kocha wake, Jose Mourinho ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu na kuwa nafasi kubwa ya kurejea Stanford Bridge kuinoa Chelsea.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyomnukuu Rais wao, Florentino Perez wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jioni, kuwa Mourinho hatafukuzwa klabuni hapo.

Perez akasema kuwa, wamekubaliana na Mreno huyo kumaliza mkataba wao na hivuyo kuondoka Real Madrid mwishoni wa msimu huu.

Pia Rais huyo aliweka bayana kwamba hawajaanza kufanya mazungumzo na kocha yeyote kwa ajili ya kuziba nafasi ya Mreno huyo ambaye amekuwa akitajwa kuwa mbioni kurejea Chelsea.

Kwa taarifa hiyo ya klabu yake ya sasa ya kuachana naye ni wazi njia ya kurejea Uingereza imekuwa nyepesi tofauti na ilivyotarajiwa na kwamba mwenyewe amekuwa akisisitiza anatamani kurudi nchini humo kutokana na mazingira aliyokuwa nayo Madrid.

Kocha huyo amekuwa na msimu mbaya kwa mwaka huu baada ya timu yake kutoambulia taji lolote ikishindwa kufuzu fainali za Ligi ya Ulaya inayochezwa Jumamosi kwa kung'olewa na Borrusia Dortmund kwenye Nusu fainali, kufungwa Fainali ya Kombe la Mfalme na kushindwa kutetea taji kwa mahasimu wao Barcelona.

No comments:

Post a Comment