
Wachezaji wa Yanga wakishuka, mbele ni Mbuyu Twite wakishuka uwanja wa Ndege Bukoba

Nizar Khalfani nae yupo kwenye kikosi

Wachezaji wakiendelea kushuka kwenye ndege

Tayari wamekanyaga Ardhi ya Bukoba

Kama kawaida: kushoto ni Khalfan Ngassa kulia ni Niyonzima

Picha ya Pamoja Viongozi na wachezaji

Dida kushoto akipata picha ya pamoja na wenzake

Kocha mkuu wa timu ya Yanga

Asante tumefika salama kazi ni moja ...ushindi ni muhimu Kaitaba

Niyonzima akiwa na Mdau wake wa bukobasports.com

Kelvin Yondani akifurahia baada ya kutua Bukoba asubuhi hii.

Bw. Jamal kalumuna kushoto akiwa na kiongozi wa Yanga

Smart Hotel

Wachezaji wakiingia Smart Hotel

Bw. Ernest Nyambo na Jamal Kalumuna wadau wakubwa wa Yanga Bukoba. (Picha: Lenzi ya Michezo)
KOCHA Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro amewajia juu baadhi ya waandishi wa habari na kuwaambia 'msituchonganishe'.
Minziro alitoa kauli hiyo alipoigiwa simu na MICHARAZO kujua msafara mzima wa timu yao kuelekea Bukoba kuumana na Kagera Sugar siku ya Jumamosi na iwapo kama walimjumuisha beki wa kati Kelvin Yondani aliyeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba alikirofichana na kocha mkuu, Ernie Brandts kiasi cha kuvua jezi na kutupa chini kisha kususia mazoezi.
Kocha huyo, nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, alisema hakuna tukio lolote lililotokea baina ya Yondani na kocha mkuu na ndiyo maana mchezaji huyo yupo kwenye msafara wa wachezaji 21 kwa ajili ya kuivaa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba.
"Ndugu yangu huyo aliyekuambia kwamba Yondani kagombana na kocha ana yake, na ningependa kuwaambia wazi Yanga hatutaki mtuchonganishe, tupo shwari na hivi sasa tumetua Bukoba salama," alisema Minziro.
Alisema Yondani ni miongoni mwa wachezaji 21 wa Yanga walioenda Bukoba kuhakikish Yanga itaibuka na ushindi dhidi ya wenyeji wao ambao anakiri huwa wasumbufu kwenye dimba lao la nyumbani.
"Msitugombanishe kabisa, tupo shwari tayari kwa kuisulubu Kagera, tumekuja kusaka ushindi huku hivyo tuacheni," alisisitiza Minziro.
Alidokeza kuwa kwa maandalizi waliyofanya dhidi ya mchezo huo ana imani kubwa ya kuibuka na ushindi Jumamosi licha ya kutarajia upinzani mkali wa wenyeji wao hao walkiowatungua katika mechi kama hiyo ya msimu uliopita iliyochezwa Oktoba 8, 2012 ambapo Yanga walilala kwa bao 1-0.