STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 31, 2014

Simba, Azam zavuna Mil. 26


MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Machi 30 mwaka huu) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza sh. 26,455,000.
Watazamaji 4,741 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawanyo kwa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,035,508.47, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,908,686 wakati kila klabu ilipata sh. 5,460,687.63.
Uwanja sh. 2,776,620.83, gharama za mechi sh. 1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh. 1,665,972.50, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 832,986.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 647,878.19.

TFF yamlilia Dk Mziray

Jamal Malinzi

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha daktari wa tiba ya michezo, Dk. Hemed Mziray kilichotokea juzi jijini Dar es Salaam.
Dk. Mziray ambaye alikuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Manispaa ya Temeke na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA) amesafirishwa kwenda kwao mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Dk. Mziray ameshirikiana na TFF na wadau wengine wa mpira wa miguu katika masuala ya tiba na uongozi.
Alikuwa kiungo kati ya Uwanja wa Taifa ambapo mechi za kimataifa, za ligi na za kirafiki zimekuwa zikichezwa na Hospitali ya Temeke kwa wagonjwa wanaohitaji huduma zaidi, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF imetoa pole kwa familia ya marehemu Dk. Mziray, TASMA na wafanyakazi wa Hospitali ya Temeke na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Pia TFF inatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake. Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina