STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 8, 2015

YANGA YALIPA KISASI, NGASSA AKIONDOA 'GUNDU'

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/NGASSA-MRISHO.jpg
Mrisho Ngassa aliyefunga mabao yote mawili Yanga ikiizamisha Mtibwa uwanja wa Taifa
MABAO mawili ya winga machachari Mrisho Ngassa aliyetokea benchi yameiwezesha Yanga kulipa kisasi kwa Mtibwa Sugar na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ambayo awali ilionekana kuugaya mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa, ulishuhudiwa dakika 45 za kwanza mambo yakiwa magumu kwa klabu zote baada ya kutofungana bao lolote.
Hata hivyo mabadiliko yaliyofanywa na kocha Hans van der Pluijm ya kumtoa Kpah Sherman na kumuingiza Mrisho Ngassa yalizaa matunda baada ya mkali huyo kufunga mabao hayo muda mchache tangu awepo uwanjani na kuifanya Yanga kurudi katika nafasi ya kwanza.
Yanga imefanikiwa kufikisha pointyi 25 baada ya mechi 13 na kuiengua Azam ambao jana walilazimishwa sare ya 2-2 na Polisi Morogoro ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 12.
Azam inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumatano kwa ajili ya kucheza na Mtibwa Sugar katika mechi ya kiporo itakayochezwa uwanja wa Chamazi.
Magoli hayo mawili yamemwezesha Ngassa kuondoa 'gundu' baada ya kutoweza kufunga bao lolote msimu huu, kitu ambacho hakikuwa cha kawaida kwa mchezaji huypo aliyewahi kuwa Mfungaji Bora.
Wakati Azam wakiingia kambini kujiandaa na pambano lao na Mtibwa, Yanga wanatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar ili kuweka kambi kusubiri  mchezo wao wa Kombe la Shirikisho utajkaocheza Jumamosi.
Yanga itashuka dimbani Jumamosi kuumana na BDF XI ya Botswana katika mechi ya mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo kabla ya kurudiana nao wiki mbil baadaye.
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                              P   W   D    L    F    A   GD   Pts
01.  Yanga              13  07  04  02  15   07  08  25
02.  Azam               12  06  04  02  17   10  07   22
03. Polisi Moro         14  04  07  03  12   11  01  19
04. JKT Ruvu           14  05  04  05  14   14  00  19
05. Ruvu Shooting   14  05  04  05   10  11   -1  19
06. Mtibwa Sugar     12  04  06  02   13  09  04  18
07. Coastal Union     14  04  06  04  11   10  01  18
08. Kagera Sugar      14 04  06  04   11   11  00  18
09. Simba                 13  03  08  02  13   11  02  17
10. Mbeya City          13   04  04  05  09  11   -2  16
11. Ndanda Fc           14  04  03   07  13  18   -5  15
12. Mgambo JKT        12  04  02  06   06  11   -5  14
13. Stand Utd            14  02  06   06   09  17   -8  12
14. Prisons                13  01  08   04   10   12   -2  11
 

Wafungaji:
7-
Didier Kavumbagu(Azam)
6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Rashida Mandawa (Kagera Sugar)
5-
Ame Ali (Mtibwa), Danny Mrwanda (Yanga)
4-
Rama Salim (Coastal),  Simon Msuva (Yanga),  Emmanuel Okwi (Simba), Nassor Kapama (Ndanda)
3- Ally Shomari (Mtibwa),  Jacob Massawe (Ndanda), Kipre tchetche (Azam)
2-
Shaaban Kisiga, Dan Sserunkuma(Simba),  Salum Kanoni, Atupele Green (Kagera Sugar) Aggrey Morris (Azam),  Najim Magulu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Amissi Tambwe, Jerry Tegete, Mrisho Ngassa (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Heri Mohammed, Mussa Said (Stand Utd), Ally Nassor,  Malimi Busungu (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi),Yahya Tumbo (Ruvu Shooting)

No comments:

Post a Comment