STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Manchester City yaua England

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/74053000/jpg/_74053198_dzeko_reuters.jpg
Edin Dzeko (10) akiifungia City bao la tatu
MANCHESTER City imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kunyakua taji la Ligi Kuu England, baada ya mapema leo kuifumua bila huruma Southampton kwa kuicharaza mabao 4-1.
Bao la dakika tatu lililofungwa na Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Youre kwa mkwaju wa penati, liliwashtusha wageni kabla ya kulirejesha dakika ya 37 kupitia Rickie Lambert pia kwa penati.
Samir Nasir aliiongezea Man City bao dakika ya 40 kwa pasi ya David Siliva na dakika nne ya nyongeza Edin Dzeko alifunga bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Kolarov.
Bao lililowewanyong'onyesha Southampton lilizalimishwa kwenye dakika ya 81 na Jovetić  akimalizia kazi ya Jesus Navaz.

No comments:

Post a Comment