STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 31, 2014

AC Milan yaitoa nishai Real Madrid Umangani

Ronaldo na El Shaarawy wakichuana
Beki wa Madrid Nacho akimdhiobiti mchezaji wa AC Milan
Karim Benzema akifunga bao la pili la Madrid kwa mkwaju wa penati
MSHAMBULIAJI Stephan El Shaarawy aliiwezesha timu yake ya AC Milan ya Italia kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid ya Hispania katika pambano la kimataifa la kirafiki lililochezwa mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
El Shaarawy alifunga mabao mawili katika kipigo hicho kilichokuwa cha kwanza kwa vijana wa Carlo Ancelotti tangu Septemba na kuhitimisha 'ubabe' wa Madrid ambao walikuwa hawajapoteza mchezo wowote katika mechi 22 katika msimu huu.
Jeremy Menez wa Milan ndiye aliyeanza kufungua milango baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 24 kabla ya El Shaarawy kuongeza goli la pili katika dakika 31 kwa shuti kali.
Dakika nne baadaye Madrid walifanikiwa kuchomoa bao moja kupitia kwa Mwanasoka Bora Duniani, Cristiano Ronaldo kufunga akiwa ndani ya 'boksi' akimtungua kipa  Diego Lopez na kuzifanya timu ziende mapumziko Milan wakiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kushuhudiwa Milan wakiongeza bao la tatu dakika ya 49 kupitia tena kwa El Shaarawy kabla ya watokea benchi Giampaolo Pazzini na M'Baye Niang kushirikiana vyema na na Pazzini kuukwamisha mpira kimiani katika dakika ya 73 kuaindikia Milan bao la nne.
Real Madrid ilijipatia bao la pili la kujifutia machozi kupitia mshambuliaji wake wa Kifaransa Karim Benzema, aliyefunga bao kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 84.
Kwa ushindi huo AC Milan walikabidhiwa kombe lililopokewa na nahodha wake, Riccardo Montolivo.

No comments:

Post a Comment