STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 29, 2014

Waamuzi, makamisaa kutahiniwa Sept 5

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGe9znsbu8-SC-K7pcwh_X4R1keXlQEZ6eKkKsYFEcEiMd59lZ-pvZBtMypkT-3vsbM6KKk8-HTX-AtQvj4Qa97tZCeIIr-3noVEg8sxx5YnUqt3q9IZm6Ar3VB-IJWfyVSQQ5vhOcAT9D/s1600/DSC_8192.JPG
Waamuzi wanatakiwa kuwa fiti kama hivi wawapo uwanjani
MTIHANI wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wanaotaka kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu utafanyika katika vituo viwili kuanzia Septemba 5-6 mwaka huu.
Waamuzi watakaoshiriki mtihani huo ni wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa class one. Pia kutakuwa na semina wa makamishna wanaotaka kusimamia mechi za VPL na FDL ambayo itafanyika Septemba 7 mwaka huu.
Vituo vya mtihani huo ni Dar es Salaam na Shinyanga. Kituo cha Dar es Salaam ni kwa waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Kituo cha Shinyanga ni kwa waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Arusha, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Rukwa, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.
Waamuzi wote ambao wamechezesha VPL na FDL msimu wa 2013/2014 na kupata matatizo au kuondolewa kwenye ligi hawahusiki na mtihani huo.
Washiriki wanatakiwa kufika kituoni siku moja kabla.Wasimamizi ni Charles Ndagala, Israel Mujuni, Issarow Chacha, Joan Minja, Pascal Chiganga, Riziki Majala, Said Nassoro, Salum Chama, Soud Abdi, Victor Mwandike na Zahara Mohamed.

No comments:

Post a Comment