STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 4, 2014

TUNAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA EID EL HAJJ

http://holisms.in/wp-content/uploads/2014/07/eid-mubarak-images.jpgMICHARAZO MITUPU INAUNGANA NA WAISLAM WOTE ULIMWENGUNI KUWATAKIA KILA LA HERI KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA EID EL HAJJ INAYOADHIMISHWA LEO DUNIANI KOTE.
SIKUKUU HII INAHITIMISHA IBADA YA HIJJA KWA WAUMINI WA KIISLAM INA MAANA KUBWA KWA WAUMINI KATIKA KUKUMBUKA TUKIO LILILOFANYWA NA MZEE WETU NA NABII IBRAHIM (AS) CHA KUTAKA KUMCHINJA MWANAE ISMAIL (AS). KABLA YA ALLAH SUBHANNA WATAALAH KUMLETEA KONDOO TOKA PEPONI ILI ACHINJWE BADALA YA ISMAIL BAADA YA KURIDHIKA NA IMANI KUBWA ALIYONAYO NABII IBRAHIM YA KUKUBALI KUMCHINJA KIPENZI CHAKE ALIYEMZAA AKIWA NA AKARAIBIA MIAKA 100.
CHA MUHIMU KWA WAUMINI WOTE WAISHEREHEKEE SIKUKUU HII KWA KUMCHA NA KUMUOGOPA ALLAH KWA KUTOSHIRIKI KWENYE MAASI NA MAMBO YA KUMUUDHI MUNGU.
WENYE UWEZO WA KUCHINJA WACHINJE KAMA UTEKELEZAJI WA SUNNAH YA SIKUKUU HII NA WASIO NA UWEZO WAJIKURUBISHE KWA KUFURAHIA SIKUKUU NA NDUGU, JAMAA NA RAFIKI NA MAJIRANI ZAO PAMOJA NA KUTAKIANA KILA LA HERI, KULA NA KUNYWA PAMOJA SAMBAMBA NA KUWAKUMBUKA WASIO NA UWEZO WAKIWAMO YATIMA, WAJANE N.K.
EID MUBARAK!

No comments:

Post a Comment