![]() |
Kocha Mart Nooij akizungtumza huku Nahodha Nadir Haroub Cannavaro akisikiliza kwa makini |

Kocha
Mart Nooij aliyetangaza kikosi akiwa mjini Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), alisema kikosi hicho kinachodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini Jumatatu.
Wachezaji
watakaoingia kambini keshokutwa ambao waliitwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na;
Makipa: Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini
Ali (Azam).
Mabeki:Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir
Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam
(Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
Viungo: Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba
(Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna
Chanongo (Simba).
Washambuliaji: Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR
Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane
Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).
No comments:
Post a Comment