Na Kipimo Abdallah
ALIYEKUWA Katibu
Mwenezi wa Baraza la Wanawake Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) Jimbo
la Kawe, Batuli Kivuma ambaye amejiunga na chama cha Alliance for Change and
Transparent (ACT-Tanzania amesema kilichomuondoa CHADEMA ni ukabila ulioota
mizizi kwa muda mrefu.
Kivuma ambaye awali
alikuwa mwanachama wa Chama Cha Wananchi CUF alisema aliamini kuwa chama hicho
kinasimamia demokrasia jambo ambalo limeshindikana hasa ukiwa hotekei mkoa wa
Kilimanjaro.
Alisema tangu ajiunge
katika chama hicho amekuwa na juhudi za kukijenga chama hasa Kata ya Msasani na
jimbo zima la Kawe ila juhudi zake zimekuwa zikikwamishwa kwa misingi ya
ukabila.
Katibu Mwenezi huyo wa
zamani wa BAWACHA alisema katika kudhihirisha hilo alishiriki kwenye mchakato wa kugombea nafasi ya Udiwani viti
maalum mwaka 2010 ambapo alishinda ila aliondolewa kwa kigezo cha yeye ni Mdigo
na wakapewa nafasi hiyo Wachaga.
“Kusema ukweli suala la
kuhama vyama sio zuri ila inafikia mahali unashindwa kuvumilia kwani nimekuwa
nikionewa mara kwa mara katika chaguzi na ukiangalia vizuri msingi wake ni
ukabilia ambao unawabeba Wachaga” , alisema.
Kivuma alisema alikuwa akikipenda sana chama hicho
lakini ubaguzi uliopo amefikia mwisho wa uvumilivu na kwamba anahitaji
kuonyesha jitihada zake kwingine.
Alisema suala hilo la
ukabila lilikidhiri katika uchaguzi mkuu ambao ulifanyika hivi karibuni hasa
katika upande wa BAWACHA ambapo juhudi zilifanywa kuanzia ngazi ya chini hadi
Taifa.
Mwenezi huyo wa zamani
wa BAWACHA alisema hata upatikanaji wa Mwenyekiti wa BAWACHA wa sasa Halima
Mdee ulitawaliwa na ukabila ikiwa ni agizo la Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe.
"Unajua hili neno
demokrasia wanalielewa je bwana kwani kwa ufahamu wangu ni kuhakikisha kuwa
jamii inaacha pale inapofanya maamuzi yake ila huku ni kinyume",
aliongezea Kivuma.
Kivuma alisema
atahakikisha kuwa anakibomoa CHADEMA hasa katika Jimbo la Kawe ambapo amefanya
kazi za kisiasa kwa muda mrefu.
Kwa upande wake
aliyekuwa Mjumbe wa Mtaa Serikali ya Mtaa wa Matofalini Ujiji Kigoma Yassin
Mohamed alisema ni vema vyama vikatambua kuwa hakuna uadui baina yao na kuhama
chama ni haki ya mtu.
Alitolea mfano hali ya
kisiasa ilivyokuwa siku za nyuma kati ya chama na CHADEMA na CUF hali ambayo
kwa sasa haipo na vinafanya kazi pamoja.
Mohamed alisema ameamua
kujiunga na ACT-Tanzania na kuondoka CHADEMA ili kupata uhuru wa kupigania
demokrasia ya kweli.
No comments:
Post a Comment