STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 4, 2014

Kamote, Mashali kuwania mikanda ya UBO Mkwakwani Tanga

http://1.bp.blogspot.com/-7Ll7tNGzRTM/Ul4ZO5z2JmI/AAAAAAAADgE/s-flZPVKG5U/s1600/DSC06608.JPG
Allan Kamote atakayewania ubingwa wa Dunia wa UBO
Thomas Mashali
BONDIA Allan Kamote wa Tanzania anatarajiwa kupanda ulingoni siku ya Jumapili kuzipiga na Osgood Kayuni wa Malawi katika pambano la kuwania ubingwa wa Universal Boxing Organization (UBO).
Mabondia hao watapambana katika pigano la uzani wa Light la raundi 12 kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mpinzani wa Kamote, tayari ameshatua nchini tangu juzi usiku na alitarajiwa kuelekea Tanga jana ili kuwahi zoezi la kupimwa afya na uzito leo Jumamosi.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Anthony Rutta, maandalizi ya pambano hilo na mengine ya utangulizi likiwa la mabondia Thomas Mashali dhidi ya Ali Ramadhani 'Alibaba' yamekamilika.
"Bondia kutoka Malawi ameshatua nchini tayari kwa pambano lake na Kamote na maandalizi kwa ujumla ya michezo hiyo ya Oktoba 5 yanaendelea vyema, hivyo wakazi wa Tanga na maeneo ya jirani wajiandae kupata burudani," alisema Rutta.
Mabondia hao wawili walishakutana mara mbili kabla ya pambano hilo la Jumapili na mara zote Mtanzania Allan Kamote amepoteza mbele ya Kayuni na hivyo pigano la keshokutwa ni nafasi ya Kamote kujifuta aibu nyumbani.

No comments:

Post a Comment