STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 4, 2014

Arsenal bado Majanga, Ramsey aumia tena kuwakosa Chelsea kesho

http://i.huffpost.com/gen/1718401/thumbs/o-AARON-RAMSEY-facebook.jpgKIUNGO Aaron Ramsey atalikosa pambano la kukata na shoka la kesho kati ya timu yake ya Arsenal dhidi ya Chelsea sambam,ba na mechi nyingine baada ya kuthibitika kuwa ni majeruhi.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa atamkosa Ramsey kwa wiki nne au zaidi. 
Nyota huyo wa kimataifa wa Wales alipata majeruhi ya msuli wa nyuma ya paja wakati wa mchezo wa Ligi Kuu uliokwisha kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tottenham Hotspurs Jumamosi iliyopita.
Kuumia huko kunamfanya akose mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano na michezo kadhaa ya Ligi Kuu ukiwamo wa kesho dhidi ya Chelsea. 
Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti kuwa Ramsey anaweza kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne lakini Wenger amesema nadhani kiungo huyo anaweza kurejea uwanjani mwanzoni mwa mwezi ujao. 
Wenger amesema kwa mujibu wa madaktari Ramsey anaweza kuwa nje kwa muda wa wiki tatu mpaka nne hivyo yeye ameamua kuhesabu nne kabisa. 
Ramsey, 23 akiwa nje ya wiki hizo ina maana atakosa michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Chelsea, Hull City na Sunderland na pambano la ugenini la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Anderlecht.

No comments:

Post a Comment