STRIKA
USILIKOSE
Saturday, October 4, 2014
Francis Cheka kuzipiga Namibia kuwani ubingwa wa WBU
BINGWA wa zamani wa Dunia wa WBF, Francis Cheka anatarajiwa kupanda ulingoni mwishoni mwa Novemba nchini Namibia kupigana na mwenyeji wake Harry Simon katika kuwania ubingwa wa WBU.
Pambano hilo la uzito wa Light Heavy litakalokuwa la raundi 12 litachezwa Novemba 29 kwenye Uwanja wa Kuisebmond mjini Walvis Bay, nchini humo.
Cheka atakuwa na kibarua kizito kwa bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza mapambano 29 na kushinda yote, 21 yakiwa ya KO, huku akiwa hajapoteza wala kutoka sare mchezo wowote.
Mkanda huo wanaouwania ulikuwa wazi na hivyo kutoa nafasi kwa Cheka kurejesha heshima yake iwapo atafanikiwa kumpiga Simon na kutwaa taji hilo katika ardhi ya ugenini.
Kwa muda mrefu, Cheka amekuwa hafanyi vizuri nje ya Tanzania na hiyo ni nafasi yake ya kuuthibitishia umma kwamba yeye ni mkali kokote kwa kumshinda mpinzani wake.
Mara ya mwisho Cheka kupanda ulingoni ilikuwa Aprili mwaka huu alipopigna na bondia kutoka Iran, Sajjad Mehrabi na kutoka naye sare.
Cheka alitwaa mkanda wa Dunia wa WBF kwa kumchakaza Mmarekani Phil Williams Agosti mwaka jana kabla ya kupoteza ubingwa huo alipoenda kuchezea kichapo cha 'mbwa mwizi' nchini Russia kwa kupigwa KO ya raundi ya tatu na Fedor Chudinov.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment