STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 5, 2014

Mtibwa Sugar ushindi 100%, Shomar ampumulia Kavumbagu

WAKATI Mtibwa Sugar ikikwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuiengua Azam, Ally Shomari, mshambuliaji huyo wa Mtibwa amemuashia taa ya kijani Didier Kavumbagu kwa kufikisha bao la tatu kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi hiyo.
Shomari ndiye aliyeifungia Mtibwa Suigar bao pekee lililoizamisha Mgmabo JKT katika mfululizo wa mechi za ligi kuu katika pambano lililochezwa kwenue uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro.
Mtibwa imeweka rekodi ya kushinda mechi zake zote tatu na kufikisha pointi 9 na kukwea kileleni mwa msimamo wakiizidi mabingwa watetezi Azam kwa zaidi ya pointi mbili baada ya timu hiyo jana kulazimishwa suluhu na Prisons-Mbeya.
Shomari alifunga bao hilo dakika ya 10 ya pambano hilo na kufanya afikishe idadi ya mabao matatu akiwa nyuma ya Kavumbagu kwa bao moja.
Didier anaongoza msimamo akiwa na mabao manne, kisha Shomar na kufuatiwa na wachezaji wanne wenye mabao mawili kila mmoja ambao ni Ami Ali wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kisiga wa Simba, Rashid Mandawa wa Kagera Sugar na Nassor Kapama wa Polisi Morogoro.

No comments:

Post a Comment