STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 16, 2013

Golden Bush Veterani yaitafuna Moro Veterani x3

Kikosi cha Golden Bush Veterani

MABAO mawili kutoka kwa Athuman Machuppa na moja la Abuu Ntiro jumamosi yalitosha kuipa ushindi wakali wa soka la maveterani jijini Dar, Golden Bush Veterani kuitambia Morogoro Veterani nyumbani kwao kwa kucharaza mabao 3-1 katika pambano la kirafiki lililochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kwa mujibu wa msemaji wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' alisema katika pambano lao walionyesha kiwango kikubwa kama kawaida yao na kuwapeleka puta wapinzani wao na kuibuka na ushindi huo wa mabao 3-1, ikiwa wanajiandaa kuvaana na wapinzani wao Wahenga.
Timu hizo mbili 'mahasimu' zilipokutana mara ya mwisho hivi karibuni kwenye uwanja wa Kinesi na Wahenga kulala mabao 2-1, huku wachezaji na aliyekuwa mgeni rasmi Kamanda wa Polisi, Thobias Andengenye wakinyeshewa na mvua iliyonyesha siku hiyo.
Pambano la safari hii kwa wapinzani hao wa jadi linatarajiwa kuchezwa siku ya maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanzania, ambapo tayari pande hizo mbili zimeshaanza kutambiana kila moja ikitamba kuibuka na ushindi ili kulinda heshima kwa wenzake.

No comments:

Post a Comment