Rais wa Miss Utalii Tanzania |
KAMPUNI ya Africa Tourism Promotion Centre kwa kushirikiana
na kampuni ya Miss Tourism Tanzania Organisation, wameandaa tamasha la
kimataifa la Safri kuu ya Kitalii Tanzania “Tanzania Great Safari Tour 2013”
kuanzia Mwezi Agost hadi Septemba 2013 nchini Tanzania.
Lengo la kuhamasisha
vita dhidi ya Ujangili wa Wanyama Pori (Uwindaji Haramu) , Misitu (Mazingira na
Uvunaji Haramu wa Mazao ya Misitu) ,Maliasili za Baharini (Uvuvi Haramu), pia kuhamasisha
Utalii wa Ndani na kutangaza Vivutio vya Utalii waTanzania kitaifa na
kimataifa.
Tamasha hilo la Safari Kuu ya Kitalii la Tanzania Great Safari Tour
2013, litajumuisha na kuhusisha mashindando ya mbio za Nyika za Kimataifa za
ANT POACHING INTERNATIONAL MARATHON, NATIONAL PARKS INTERNATIONAL MARATHON,
WILDLIFE TOURISM INTERNATIONAL MARATHON,sambamba na msafara mkuu wa kitalii
Tanzania wa kutembelea na kupiga picha za Televisheni, Video, Filamu na Minato
za Makala, Matangazo, Magazeti, Majarida, Tovuti, Mitandao ya Kijamii na
vipindi maalum vya Televisheni,Redio na Filamu.
Tanzania ni miongoni mwanchi chache Duniani zilizojaliwa
kuwa na vivutio vingi na vya pekee vya Utalii Duniani, kuanzia Hifadhi za
Taifa, Mapori ya Akiba, Hifadhi za Bahari, Maeneo ya Kihistoria, Maajabu ya
Dunia, Hifadhi za Wanyama Pori na Utajili mkubwa wa Utamaduni wa kuvutia.
Ndiyo
maana sekta ya Utalii nchini ni moja ya sekta tegemezi na kiongozi katika pato
la Taifa na kuingiza fedha za kigeni. Utalii unachangia zaidi ya 18% ya pato la
Tifa, 24% ya Pato la fedha za kigeni la Taifa na zaidi ya 12% ya ajira zote
nchini kila mwaka.
Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kukuza
na kuendeleza sekta ya utalii nchini, ikiwa ni pamoja na juhudi kubwa za
kutangaza Utalii na vivutio vya utalii vya Tanzania kitaifa na kimataifa lakini
pia kulinda na kuhifadhi maliasili za Taifa za Utalii, kupitia wizara ya
maliasili na utalii na mamlaka zake tanzu za Utalii nchini,ikiwemo Bodi ya
Utalii(TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro(NCAA), Mamlaka ya Huduma za Misitu (Tanzania Forest Services), Mamalaka
ya Wanyama Pori na Mamlaka ya Hifdhi ya Mambo Kale.
Juhudi hizo sasa zimezaa
matunda katika kukuza utalii nchini tofauti na miaka ya nyuma, hata hivyo
pamoja na mafanikio hayo sekta ya Utalii nchini sasa inakabiliwa na changamoto
nyingi ,lakini kubwa ikiwa ni Ujangili wa uwindaji Haramu na Uvunaji Haramu wa
Mazao ya Misitu na Majini, lakini pia changamoto ya Utalii wa Ndani na
Utangazaji wa Vivutio vya Utalii Kitaifa na Kimataifa.
Changamoto hizi hasa ya Ujangili, imekuwa ni tishio kubwa kwa
ustawi na ukuaji wa sekta ya Utalii nchini, kutokana na kukua na kuongezeka kwa
uwindaji haramu na uvunaji wa nyara za maliasili za misitu na bahari, ambayo
sasa imekuwa ni janga la Taifa na tishio la kutoweka kwa baadhi ya wanyama Pori
,Viumbe Bahari na Misitu. Tunaamini kuwa, wakati sasa umefika ,tena wakati
sahihi kwa sekta Binafsi kuungana na sekta za Umma katika kupigana na
kuhamasisha vita dhidi ya uwindaji Haramu,Uvuvi Haramu na Uvunaji haramu wa
Misitu nchini, lakini pia katika kutangaza vivutio vya utalii Kitaifa na
kimataifa na pia kuhamasisha utalii wa Ndani.
Kutokana na kukua kwa sekta ya
Utalii Duniani na kuwa moja ya sekta muhimu katika uchumi Duniani, mataifa
mengi duniani na Afrika ikiwemo Tanzania
na nchi jirani na Tanzania zimewekeza kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa sana
katika ushirikiano na uungaji mkono wa hali na mali wa juhudi za asasi binafsi
za kutangaza na kupromoti utalii na vita
dhidi ya Ujangili kama Africa Tourism Promotion Centre na Miss Tourism Tanzania
Organisation.
Tanzania Great Safari Tour ni jibu na tafsiri ya vitendo ya
sera za taifa za Utalii, Wanyama Pori, Misitu na Utamaduni, ambapo matukio ya
kimataifa ya Mbio za Nyika za Ant Poaching International Marathon, National
Parks Marathon, Wildlife Tourism International Marathon, sambamba na ziara ya
washiriki wa kitaifa na kimataifa wa Tanzania Great Safari Tour, katika Hifadhi
za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Maeneo ya Kihistoria, Maeneo ya
Kitamaduni, Maeneo ya Hifadhi za Bahari, Maeneo ya Hifadhi za Misitu na Vivutio
vingine vya Utalii nchini, huku wakihamasisha vita dhidi ya UJangili,
wakihamasisha Utalii wa Ndani, Utalii wa Kitamaduni, Utalii wa Mikutano, Utalii wa
Mazingira na kutangaza Vivutio vya Utalii vya Tanzania Kitaifa na Kimataifa.
Tanzania
Great Safari Tour 2013, ni Safari Kuu ya Kitalii ya Kihistoria likiambatana na
ushiriki mkubwa wa vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, ambayo itawaweka
na kuwakutanisha pamoja wasanii wa kitaifa na kimataifa wa Filamu, Urembo, Mitindo, Muziki, Ngoma
za Asili na Maigizo lakini pia wanamichezo wa kitaifa na kimataifa wa Mpira wa
Miguu, Riadha, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Meza, Rugby sambamba
na wanadiplomasia na waandishi wa Habari wa
Televisheni, Redio, Magazeti, Makala, Majarida na Mitandao ya Kijamii kitaifa na
kimataifa.
Tanzania Great Safari Tour 2013, ni fulsa nyingine kwa
Tanzania kutangaza Utalii na Kuhamasishisha Vita Dhidi ya Uwindaji Haramu,Uvuvi
Haramu, Uharibifu wa Mazingira na Ujangili kwa Ujumla, kwani matukio yote ya
Tanzania great Safari Tour 2013 yataonyeshwa na kurushwa moja kwa moja (LIVE)
kutoka Tanzania na kuonekana Duniani kote kupitia Televisheni, Tovuti, Internet
na Mitandao ya Kijamii, huku Promo DVD na DVD za Filamu ya ziara zima
zikigawanywa Katika vyombo mbalimbali vya habari na Taasisi za
Kidiplamasia, Mashirika ya ndege, Vyuo Duniani kote.
Matukio katika zira
hiyo ni pamoja na Mbio Live za Ant Poaching International Marathon 2013,
National Parks International Marathon 2013, Wildlife Tourism International
Marathon 2013, Great Safari Wildlife Fashion & Talent Show 2013, Ant
Poaching Street Carnival 2013, Great Safari Ant Poaching Sports Bonanza 2013 na
Mdahalo wa kitaifa wa Ujangili, Utalii na Utalii wa Ndani. Washindi wa fainali
za Taifa za Miss Utalii Tanzania , watashiriki katika Tamasha hilo ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya kwenda kushiriki katika mashindano ya Dunia ya Miss
Tourism World 2013 huko Equatorial Guinea Octoba mwaka huu na Miss Tourism
United Nation 2013 huko Florida Marekani Novemba mwaka huu.
Kaulimbiu ya Tamasha la Tanzania great Safari Tour 2013, ni “Stop
Poaching, Protect Wildlife – Tourism is Life, Culture is Living” (Piga Vita
Ujangili, Linda Wanyama Pori – Utalii ni Maisha, Utamaduni ni Uhai wa Taifa).
Asante.
Erasto Gideon Chipungahelo
Mwenyekiti Mtendaji
Africa Tourism Promotion Centre na Miss Tourism Tanzania
Organisation
No comments:
Post a Comment