STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, July 14, 2013

Wajumbe TFF wapitisha Katiba Mpya


Mwakilishi wa FIFA katika mkutano huo wa TFF, James Johnson akihutubia

Rais Leodger Tenga na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah wakiwa na Mwakilishi wa FIFA, James Johnson,


 

Baadhi ya Wajumbe wa TFF katika mkutano huo

Na Boniface Wambura
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) uliofanyika jana (Julai 13 mwaka huu) wamepitisha marekebisho ya Katiba yake, hivyo mchakato wa uchaguzi unatarajia kuanza wakati wowote.

Wajumbe zaidi ya 100 walihudhuria Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa NSSF Waterfron, Dar es Salaam na kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aliyewataka wajumbe kuhakikisha kiwango cha mpira wa miguu nchini kinakuwa.

Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga umefanya marekebisho ya Katiba kutokana na maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). James Johnson kutoka Idara ya Wanachama ndiye aliyeiwakilisha FIFA katika mkutano huo.

Aprili mwaka huu FIFA ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF, na kuagiza kwanza yafanyike marekebisho ya Katiba ili kuingiza Kamati ya Maadili, na Kamati ya Rufani ya Maadili ambavyo ndivyo watashughulikia matatizo ya kimaadili kwa familia ya mpira wa miguu nchini.

Mbali ya kamati hizo, mabadiliko hayo pia yametengeneza ngazi mbili za kushughulikia masuala ya kinidhamu ambazo ni; Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Rufani ya Nidhamu.

Kamati ya Utendaji ya TFF chini ya Rais Tenga itakutana kesho (Julai 14 mwaka huu) kwa ajili ya kuteua wajumbe watakaounda Kamati hizo ili kuruhusu kuanza mchakato wa uchaguzi ambao FIFA iliusimamisha hadi vitakapoundwa vyombo hivyo.

No comments:

Post a Comment