STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 13, 2013

Taifa Stars bado sana, yapigwa na The Cranes




LICHA ya ahadi tamu toka kwa kocha Kim Poulsen na kauli ya Rais wa TFF, Leodger Tenga kwamba timu ya taifa, Taifa Stars imeiva kwa mashindano, hali imekuwa tofauti jioni hii baada ya Stars kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Uganda the Cranes katika mechi ya mkondo wa kwanza ya kuwania kucheza CHAN.
Stars ikiwa na nyota wake karibu wote ukiondoa wawili tu wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ambao haruhusiwi kuitumikia timu hiyo, ilikubali kipigo hicho kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao lililoizamisha Stars na kuwa na wakati mgumu kwenda kuiondosha The Cranes nyumbani kwao wiki ijayo liliwekwa kimiani na Iguma Dennis dakika moja tangu kuanza kwa kipindi cha kwanza.
Stars inaweza kujilaumu kwa kukosa mabao mengi ya wazi kutokana na nafasi zilizopotezwa na washambuliaji wake huku ikionekana kupwaya katika kiungo kusiko kawaida.
Kwa kipigo hicho Stars italazimisha kupata ushindi usiopungua mabao 2-0 iwapo inataka kuing'oa Uganda na kwenda Afrika Kusini mwakani kwenye Fainali hizo za timu za taifa zinazohusisha wachezaji wa ndani tu.
Pia ni kipigo cha tatu mfululizo kwa Stars baada ya vile ilivyopata katika michezo yake miwili ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za mwakani zitakazochezwa Brazili kwa kulala mbele ya Morocco kisha kucharazwa na Ivory Coast katika mechi zao za kundi C.

No comments:

Post a Comment