Na Boniface Wambura
PAMBANO la kwanza la mchujo la kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa
Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na
Uganda (The Cranes) iliyochezwa jana (Julai 13 mwaka huu) limeingiza sh.
113,268,000 kutokana na watazamaji 17,121.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) ni sh. 17,278,169.49 wakati wa gharama za uchapaji
tiketi ni sh. 7,809,104.
Asilimia
15 ya uwanja sh. 13,227,108.98, asilimia 20 ya gharama za mechi sh.
17,636,145.30 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 4,409,036.33.
Asilimia
60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 52,908,435.91 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,645,421.80
ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
No comments:
Post a Comment