Rais wa TFF, Leodger Tenga akiwahutubia kwenye mkutano wa jana wa TFF |
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa michango yao, na utulivu waliouonesha katika kupitisha marekebisho ya Katiba ya TFF ya 2013.
Amesema marekebisho hayo yatawasilishwa kesho (Julai 15 mwaka huu) kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kwa ajili ya kupitishwa ili mchakato wa uchaguzi uweze kuanza mara moja.
“Tutamuomba Msajili atusaidie kusajili haraka Katiba yetu ya 2013 ili tuingie katika mchakato wa uchaguzi. Kama tulivyotangaza awali tumepanga kufanya uchaguzi Septemba 29 mwaka huu, na tusingependa tarehe hiyo ipite,” amesema Rais Tenga wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji.
Katika kikao chake, Kamati ya Utendaji imepitisha Kanuni za Maadili, Kanuni za Nidhamu, na marekebisho kwenye Kanuni za Uchaguzi yanayotokana na kuundwa kwa Kamati ya Maadili.
No comments:
Post a Comment