Kocha Kim Poulsen (Kati) |
kiri kwamba vijana wake hawakustahili kupoteza mechi
Akizungumzia matokeo hayo baada ya mchezo huo, Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesema mpira wa miguu ni mchezo wa kufunga mabao ambapo timu ilipata nafasi nzuri katika dakika ya kwanza tu lakini ilishindwa kuibadili kuwa bao.
“Uganda walitengeneza nafasi moja tu katika kipindi cha kwanza wakati sisi tulikuwa nazo kadhaa. Kipindi cha pili tuliwapa nafasi wakafunga bao lao. Lakini kwa kifupi kama wao wameweza kufunga hapa (Dar es Salaam), hata sisi tunaweza kufunga Kampala,” amesema Kim akizungumzia nafasi ya timu yake kusonga mbele.
Timu hizo zitarudiana jijini Kampala kati ya Julai 26 na 27 mwaka huu ambapo mshindi ndiye atakayepata tiketi ya kwenda kwenye fainali za tatu za CHAN zitakazofanyika Afrika Kusini. Stars ilicheza fainali za kwanza za CHAN zilizofanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
Katika hatua nyingine baadhi ya wadau wa kandanda walikiponda kikosi cha Stars kwa mchezo wa jana kwa kudai ni kama hawakujua walikuwa wanatakiwa kufanya nini uwanjani.
Kipa wa zamani wa kimataifa wa Simba ambaye kwa sasa ni kocha, Spear Mbwembwe alisema hajawahi kuona Stars ikicheza kichovu kama mechi ya jana, akisema kwa mtazamo wake ni wachezaji wawili tu waliokuwa wakitimiza wajibu ambao ni winga Mrisho Ngassa na beki Aggrey Morris.
"Wengine hawakuwa mchezoni kabisa na kibaya zaidi mabadiliko yaliyofanywa ya kutolewa kwa Nyoni na kuingiwa Luhende wakati nilidhani Kapombe na Nyoni wangebadilishana nafasi tu na tumeona kilichotokea," alisema.
Mbwembwe alisema ni lazima Stars ifanye kazi ya ziada kwa mechi ya marudiano aliyoikatia tamaa kwa madai haoni kitakachobadilisha matokeo ikizingatiwa wachezaji ni wale wale na kocha yule yule tena ugenini.
"Mie nadhani kuna haja TFF ikafanya jambo moja la muhimu, lazima Poulsen apewe kocha ambaye yupo 'active', sidhani kama Sylveter Marsh anamfaa kocha wakati kwa miaka miwili sasa hana timu yoyote anayofundisha," alisema Mbwembe.
Kocha huyo alisema tatizo la kubebana ndilo linalogharimu ska la Tanzania kusonga mbele licha ya mikakati mizuri na kocha bora iliyonayo Tanzania, yaani Kim Poulsen kutoka Denmark.
Kipigo cha jana ni cha tatu mfululizo kwa Tanzania baada ya vipigo viwili vya awali toka Morocco na Ivory Coast walioumna nao katika mechi za marudiano ya kuwania Fainali za Kombe la Dunia za Brazili.
No comments:
Post a Comment