STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 13, 2015

Jinamizi la Sikinde videoni, Valentine wapo Pentagone

BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Mlimani Park 'Sikinde' imerekodi video ya wimbo wao mpya uliobeba jina la albamu ya ijayo iitwayo 'Jinamizi la Talaka',  huku wakiweka bayana kwamba watajumuika na mashabiki wao kusherehekea 'Siku ya Wapendanao' jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa viongozi wa Sikinde, Abdallah Hemba, aliiambia MICHARAZO kuwa bendi yao imerekodi video hiyo ambayo ipo hatua za mwisho kukamilishwa kama utambulisha wa ujio wa albamu yao mpya itakayokuwa na nyimbo saba.
Hemba ambaye ni mmoja wa waimbaji nyota nchini alisema kuwa mara video hiyo itakapokamilika wataiachia hewani na kuanza jukumu la kumalizia nyingine za nyimbo zilizosalia kabla ya kufanya uzinduzi baadaye mwaka huu.
"Tumeanza kurekodi video za nyimbo za albamu yetu mpya, tumeanza na 'Jinamizi la Talaka' ikiwa hatua za mwisho na tutaendelea kwa nyingine baadae," alisema Hemba.
Hemba alisema katika kusherehekea Siku ya Wapendanao itakayoadhimishwa kesho, bendi yao itafanya onyesho maalum kwa wakazi wa Kurasini eneo la Mivinjeni katika ukumbi wa Pentagone Pub.
"Tutajumuika na mashabiki wetu eneo la Mivinjeni Kurasini kwa kutambulisha nyimbo mpya na kuwakumbushia za zamani ili kuonyesha tunawapenda katika ukumbi wa Pentagone Pub," alisema Hemba, aliyewahi kutamba na bendi ya Mchinga Sound.

No comments:

Post a Comment