STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 13, 2015

Mume wa Bobby Kristina kizimbani adaiwa kumpiga

Bobby Kristina

Bopbby na mumewe Nick Gordon
NEW YORK, Marekani
MUME wa msanii Bobby Kristina, Nick Gordon, anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu shitaka la makosa ya uzembe barabarani.
Pia mamalaka nchini hapa zinamchunguza kwa tuhuma za kumjeruhi, Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa mwanamuziki nguli wa zamani, Whitney Houston.
Marehemu Whiyney alizaa mtoto huyo na mwanamuziki mwingine mahiri, Boby Brown, ambaye ni gwiji wa kutumia dawa za kulevya.
Mahakama ya Fulton County State, leo inatarajia kutoa kibali cha kukamaktwa kwa Gordon iwapo atashindwa kuhudhuria kesi ya awali inayomkabili.
Mahakama hiyo inatarajia kutoa kibali hicho ikiwa ni wiki moja tangu Bobbi Kristina, alipokutwa amepoteza fahamu bafuni huku kichwa chake kikiwa ndani ya sinki lililokuwa limejaa maji.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, polisi wa mjini hapa wamesema wana imani Gordon alimjeruhi mkewe kabla ya kutokea tukio hilo.
Tayari polisi wameanza kuchunguza mienendo ya uhusiano wa wawili hao, kabla ya Bobbi Kristina, kukutwa na tukio hilo, Jumamosi wiki iliyopita.
Aidha, mamlaka ya kiuchunguzi zimedai wanandoa hao wamekuwa na historia ya kushambuliana ambapo dakika 15 kabla ya tukio hilo walinaswa wakiwa kwenye malumbano makali.
Max Lomas ambaye ni rafiki wa Bobbi Kristina, alidai Gordon alifuta damu katika eneo la tukio zinazosadikiwa kuwa za mkewe.
Lomas alidokeza kuwa alilazimika kuingia nyumbani kwa Bobbi Kristina, baada ya kugonga mlango kwa muda kabla ya kuingia ndani baada ya kukosa mtu wa kumfungulia na kumkuta rafiki yake akiwa amepoteza fahamu bafuni.
Waaguzi katika hospitali aliyolazwa msanii huyo wa vipindi vya televisheni, wanasema hali yake sio nzuri na mjomba wake ameandika kwenye mtandao wa Instagram kuwa hali ya mpwa wake haileti matumaini.
Mjomba huyo alisema madaktari walimwambia ajiandae kupokea taarifa yoyote kwa kuwa hakuna matumaini Bobbi Kristina, kuokoa uhai wake. 
Hatua ya kupoteza fahamu, Bobbi Kristina, limeushtua ulimwengu kwa kuwa linafanana na tukio la kifo cha Whitney aliyefariki Februari 12, 2012.
Whitney alikutwa amefariki bafuni katika Hoteli ya Beverly Hilton huku kichwa chake kikiwa ndani ya maji.
Katika tukio hilo, polisi walikuta chupa za pombe, vyeti vya hospitali vilivyokuwa vikionyesha kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo na matumizi ya dawa za kulevya aina ya kokein.
Gordon na Bobby Kristina, walifunga ndoa Januari, mwaka jana licha ya ndoa hiyo kupingwa vikali na Bobby Brown kwa kuwa Godon ni mtoto wa kuasili wa Whitney.

Katika hatua nyingine imeelezwa kuwa mwanadada huyo ameanza kufumbua macho, ikiwa ni kwa mujibu wa shangazi yake.

No comments:

Post a Comment