STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 13, 2015

Mashindano ya Darts kuanza leo Dar

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhVhKfp8h_7sD24sQdW1fxe6itt9YmYbhqVgfkjiu_DA4OxDGKyiOAFD50V8_-ANUr9zuzNVqcLlfoJ7LFfThDq0B_g8qGB_iA4hrLwXtADp89WPM687LH0H_5Sjk-6LfEsGib4q9crHIc/s1600/IMG_4856.jpgMASHINDANO ya mchezo wa vishale (darts) yatakayoshirikisha timu kutoka nchi Tanzania, Kenya na Uganda, yajulikayo kama ‘Kaunje Memoriam Floating Cup’, yanaanza kutimua vumbi leo kwenye Hoteli ya Moshi, Manzese jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na mabingwa wa 2014 wa Afrika Mashariki, Klabu  ya Frendz ya Kinondoni kwa usimamizi wa chama cha mchezo huo Taifa (Tada), yatafanyika kwa siku tatu mfulizo na kufikia kilele chake keshokutwa.
Katibu wa Klabu ya Frendz, Nimesh Katakia alisema kuwa mashindano hayo ni maalum kwa ajili ya kuwaenzi waliokuwa waanzilishi wa klabu hiyo ambao ni marehemu, Kaushik Nariadhara na Said Njenga.
Alisema mashindano hayo yatachezwa kwa mtindo wa timu, wachezaji wawili wawili na mchezaji mmoja mmoja (wanaume), na kwa wanawake yatachezwa kwa mtindo wa timu na mchezaji mmoja mmoja.
Bingwa wa mashindano hayo kwa upande wa timu (wanaume), alisema atajinyakulia fedha taslim Sh. 300,000,  vikombe viwili huku kimoja kikiwa ni cha kushindaniwa kila mwaka, medali sita na cheti. Mshindi wa pili ataibuka na Sh. 200,000, kikombe na cheti wakati mshindi wa tatu ataondoka na Sh.100,000 na cheti.
Aliongeza kuwa, bingwa kwa upande wa wachezaji wawili wawili (wanaume), ataondokana Sh.100,000, medali  na cheti na mshindi wa pili atazawadiwa Sh. 50,000 na cheti, wakati bingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) atajinyakulia Sh.100,000, medali, kikombe na cheti na mshindi wa pili atazawadiwa Sh.50,000 na cheti.
Alisema kwa upande wa timu (wanawake),bingwa atazawadiwa Sh.50,000, kikombe, medali na cheti na mshindi wa pili ataibuka na Sh.30,000 na cheti, wakati bingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja, atajinyakulia Sh.30,000, kikombe na medali na mshindi wa pili ataambulia Sh.20,000 na cheti.

No comments:

Post a Comment