STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 13, 2014

Steve Nyerere atema cheche Bongo Movie

Steve Nyerere (kushoto) akiwa na Mkwere kwenye msiba wa Mzee Small
MWENYEKITI wa Bongo Movie, Steve Nyerere amesema umefika wakati wasanii wa filamu nchini na waigizaji kwa ujumla kujenga utamaduni wa kupenda kusaidiana wakati wanapokuwa na shida badala ya kuonyesha umoja na mshikamano kwenye misiba tu.
Steve alisema wasanii wamekuwa wepesi kujitokeza na kuonyesha umoja na mshikamano kwenye mazishi ya wenzao, lakini wamekuwa wazito wakati wasanii wenzao wanapokuwa na matatizo ikiwamo kuugua au janga lolotge linalowapata kitu ambacho alidai siyo kizuri.
Akizungumza na MICHARAZO kwenye msiba wa Mzee Small, Steve Nyerere ambaye majina yake kamili ni Steven Mengele alisema ni aibu wasanii na wadau wa sanaa kuchangishana fedha wakati wa misiba ya wenzao wakati wanapokuwa wagonjwa wanashindwa kutoa fedha kuwasaidia kuokoa uhai wao.
Muigizaji huyo na muigaji wa sauti za watu mashuhuri duniani, alisema anajisikia aibu na kujifunza mambo mengi kupitia msiba wa Mzee Small ambaye amekufa huku akisononeka kutengwa na waigizaji wenzake wakati akihitaji msaada wa matibabu.
"Ifike wakati wasanii sasa tukajenga utamaduni wa kusaidiana wakati wa matatizo, Mzee Small alikuwa anaugua naamini fedha ambazo zinatumika leo kugharamia mazishi yake ingetosha kusogeza uhai wake hata kama kifio kimeumbwa kwa kila mtu na hakuna wa kuweza kuzuia kisimfikie yeyote," alisema.
Alisema tayari chini ya uongozi wake wameunda mfuko wa kusaidia wasanii wenye matatizo na wapo katika mchakato wa kufanya mazungumzo na taasisi za kijamii na fedha kama NSSF, PSPF na GPRF na Bima ya Afya ili kuwezesha wasanii kujiunga nayo na kujiwekea akiba inayoweza kuwasaisdia wanapokuwa wamekwama.
"Pia kama wazo alililotoa Mkuu wa Mkoa, Meck Sadick wakati wa kuagwa marehemui George 'Tyson' Otieno juu ya kuanzisha Saccos au benki tunalifanyia kazi na Inshallah mambo yakikaa vyema tutaanika kila kitu hadharani, kwa sababu hali inatosha na wasanii wamekuwa wakiumia wanapokumbwa na matatizo kama haya," alisema

No comments:

Post a Comment