STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 13, 2014

Fabregas atua rasmi Chelsea kama utani

CHELSEA wamekamilisha usajili wa kiungo wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas kutoka Barcelona kwa ada ya uhamisho inayoaminika ya paundi milioni 30 na amesaini mkataba wa miaka mitano.
Fabregas aliiambia tovuti rasmi ya klabu hiyo: "Kwanza napenda kumshukuru kila mmoja klabuni FC Barcelona ambako nimefurahia miaka mitatu mizuri. Ilikuwa ni klabu yangu ya utotoni na daima nitajivunia kwamba nilikuwa na fursa ya kuchezea timu kubwa kiasi hicho.
"Najiona bado nina kazi ambayo sijaimaliza katika Ligi Kuu ya England na sasa ni wakati mwafaka kurejea.
"Nilitafakari ofa nyingine zote kwa umakini na nikaona kwamba Chelsea ni chaguo bora. Wanalingana na malengo yangu ya soka kutokana na njaa yao ya kutwaa makombe. Wana kikosi cha wachezaji wazuri na kocha babkubwa. Nimeingia kikamilifu katika timu hii na nashindwa kuendelea kusubiri kuanza kazi."
Fabregas alifunga magoli nane katika La Liga akiwa na Barcelona na kutoa pasi za mwisho zilizozaa magoli 19 katika mechi 36 msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment