STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 7, 2015

Mnyama ashindwa kutamba Tanga, Azam yarudi kileleni

* Kagera Sugar yaondoa gundu Shinyanga, Ndanda bado sana nyumbani

http://4.bp.blogspot.com/-HlzYMgUqY6E/VLYmO19_SFI/AAAAAAAAw04/Tum0BDfocyc/s1600/simba-mapinduzi_2015.jpg
Simba iliyong'ang'aniwa Tanga
http://api.ning.com/files/cPakA0chAEyfyqjZRP3k2djpZ9GyxNW23W69D7FY4fYhsuNz2vmH6gr7yEITcci18IdnTvIgOej4xydmYu8LtJiXW0uQDhCL/16.jpg
Kagera Sugar waliooindoa 'gundu' kwa kushinda uwanja wa Shinyanga
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVRbEIHy7_801zrOMtfyS9oWnAn9Wj6oTahWAMqqpwD5pn_QaYj-Kl6fpolmlrZ0fr5VQYOEkeiFe9NflY7atBcCjdsvEREiubcYjodwWeAlUxWTreYDXgIRhZmXPJQjkX7wMXw95djYBf/s1600/10847549_808297752551709_8272495318791573431_o-790072.jpg
Azam waliorejea kileleni kwa muda baada ya sare ya 2-2 mjini Morogoro
MDUDU wa sare ametawala katika viwanja vitano wakati wa michezo ya  Ligi Kuu Tanzania Bara zilizochezwa jioni ya leo, 'Mnyama', Simba alishindwa kufurukuta Tanga na Azam wakang'anganiwa Morogoro.
Simba ikicheza na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani walitoka suluhu, wakati Azam walitoshana nguvu na Polisi Moro kwa kutoka sare ya mabao 2-2.
Magoli katika pambano la mjini Morogoro, mabingwa watetezi walipata mabao yake kupitia kwa mapacha Kipre Tchetche  dakika 10 na Kipre Balou dakika 66 kwa frikiki.
Polisi walipata mabao yake kupitia Edward Christopher katika dakika ya 25 na Selemen Kassim Selembe' dakika ya 69.
Katika uwanja wa Chamazi, JKT Ruvu na Mbeya City walitoka sare ya bao 1-1, matokeo yaliyofana na yale ya mjini Mtwara kati ya Ndanda Fc dhidi ya wageni wao Stand United.
Wenyeji walishtushwa kwa bao la dakika ya 9 la wageni lililofungwa na Jibelele Abasilim kabla ya kuja kusawazisha katika dakika ya 53 kupitia kwa Nassor Kapama.
Mjini Mbeya, wenyeji Prisons ilishindwa kutamba Kwenye uwanja wa Sokoine, baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting.
Ruvu walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa Yahya Tumbo kwa tiktak kabla ya wenyeji kusawazisha dakika ya 36 kupitia kwa  Jacob Kalipalate na kuzifanya timu hizo zigawane pointi moja moja.
Kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga, Kagera Sugar waliondoa gundi baada ya kuicharaza Mgambo JKT bao 1-0. Bao hilo liliwekwa kimiani na Atupele Green.
Ushindi huo umeifanya Kagera kufikisha pointi 18 na kuzidi kuifanya ligi hiyo kuwa ngumu kutokana na klabu kufungana au kutofautiana kwa pointi chache, Azam wakirejea kileleni wakiiengua Yanga.
Licha ya timu zote kuwa na pointi 22 Azam wanaongoza kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, huku Mtibwa wakiporomoka kutoka  nafasi ya tatu hadi ya sita.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa pambano moja tu kwenye uwanja wa Taifa, Yanga ikivaana na Mtibwa Sugar katika mechi ya kisasi kwani Mtibwa waliitoa nishai Yanga kwenye uwanja wa Morogoro kwa kuifunga mabao 2-0 katika mechi ya ufunguzi wa ligi ya msimu huu uwanja wa Jamhuri.

No comments:

Post a Comment