STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 7, 2015

Nyosso, Morris wafungiwa kisa 'uhuni' uwanjaniSHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limefungua makucha yake na kumuadhibu beki ngangari wa Mbeya City, Juma Nyosso kwa kitendo cha kumshika mshambuliaji wa timu yake ya zamani, Simba Elias Maguri.
TFF imemfungia Nyosso adhabu ya mechi nane na klabu yake imesema itakata rufaa kwa mabai ni ya kionevu na yenye kuviza maendeleo ya soka hata kama ni kweli beki wao alifanya kitndo hicho kinavyotafrisiwa kuwa ni 'udhalilishaji'.
Nyosso anatuhumiwa kumfanya 'ubasha' Maguri timu zao zilipokutana January 28 na Simba kulala mabao 2-1.
Mbali na Nyosso pia TFF imemfungia mechi tatu beki mahiri wa Azam, Aggrey Morris kwa madaiu ya kumpiga kiwiko kilichomfanya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kuzimia uwanjani.
Morris anadaiwa kufanya tukio hilo wakati timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Taifa Januari 25 na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Beki mwingine George Assey anayedaiwa kumpiga kabali Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe yeye amewekwa kiporo kwa kushindwa kuhudhuria kikao cha kamati ya Nidhamu iliyotoa adhabu hizo.
Assey anayeichezea Ruvu Shooting alionekana akimniga na kumtoa damu Tambwe katikia mechi yao kwenye uwanja wa Taifa iliyoisha kwa sare isiyo na magoli.

No comments:

Post a Comment