STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 7, 2015

Cannavaro aomba radhi askari aliyemkumbatia Mkwakwani

http://4.bp.blogspot.com/-pxH2-GRW39I/UxgIPhAR70I/AAAAAAAAKTM/vAosaujzMrY/s1600/CANNA.tif
Nadir Haroub 'Cannavaro'
NAHODHA wa klabu ya Yanga na mfungaji wa bao pekee la Yanga wakati wanaizamisha Coastal Union nyumbani Mkwakwani Tanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amemuomba radhi askari aliyemkimbilia na kumkumbatia dakika chache baada ya kufunga.
Cannavaro alifunga bao hilo katika dakika ya 11, Jumatano iliyopita na kufanya kitendo hicho ambacho kilikuwa gumzo.
Cannavaro alisema alimuomba askari huyo msamaha muda mfupi baada ya mechi hiyo ambapo aliamua kumfuata na kumueleza kuwa hakuwa na nia mbaya.
Cannavaro alisema anamshukuru askari huyo kwa kukubali maombi yake ya msamaha aliyoyatoa kwani hakutarajia hali hiyo kutokea kutokana na furaha aliyoipata baada ya kufunga bao hilo.
“Kiukweli nilifanya kosa kukimbia na kwenda kumkumbatia askari wakati nashangilia bao nililolifunga, nilijikuta ghafla nafanya kitendo kile bila kutarajia, sikukitarajia kabisa wala sikupanga iwe hivyo.

“Baada ya mechi kumalizika nilimfuata nikazungumza naye, pia walikuwepo baadhi ya viongozi wangu na wale wa polisi niliwaomba radhi kwa kitendo hicho nilichokifanya, nikashukuru wakanielewa na kulimaliza tatizo hilo,” alisema Cannavaro. 
Saleh Jembe

No comments:

Post a Comment