STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 28, 2014

Kumekucha Tamasha la Busara 2014


Picha wa tatu kulia,ni Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara Promotions,Bwa.Simai Mohamed akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun,jijini dar kuhusiana na ujio wa tamasha la muziki la Sauti za Busara la 11 katika kusherehekea utamaduni na muziki wa Afrika.Bwa.Simai amefafanua kuwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika kuanzia tarehe 13 mpaka februari 16 katika viwanja vya kihistoria vya Ngome Kongwe,Zanzibar.

Jumla ya Vikundi 32 vitafanya maonyesho jukwaani kwa asilimia 100 live.Bwa Simai amesema kuwa vikundi hivyo vimechaguliwa kutokana na maombi zaidi ya 560 na vinawakilisha nchi 19,ameongeza kuwa zaidi ya wasanii 200 watafika Zanzibar kufanya maonyesho ya muziki,wasanii hao wanatoka Afrika Mashariki,Afrika Kusini na Magharibi,maeneo ya mto Nile na pia kutoka Puerto Rico.

Kutoka Tanzania,Wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Jhikoman,Ashimba,Swahili Vibes,Hoko Roro,Seven Survivor,Abantu Mandingo,Segere Original na Kazimoto.

Pichani ni Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo,aitwaye Jhiko Man pichani akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.

Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara,aitwaye Ashimba pichani nae akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
Kwa Tarifa mbalimbali za tamasha hilo tembelea www.busaramusic.org.

No comments:

Post a Comment