STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 1, 2013

Zahoro Pazi akwama 'bondeni' Mzimbabwe amzidi kete Bloemfotein Celtic

Pazi (kulia) alipokuwa Azam kwenye mazoezi ya timu hiyo


MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu za Mtibwa na Azam aliyetua JKT Ruvu kwa mkopo, Zahoro Pazi, amekwama kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini alipoenda kujaribiwa kwa siku 10 katika klabu ya Ligi Kuu ya Bloemfotein Celtic.
Akizungumza na NIPASHE, Pazi aliyerejea usiku wa kuamkia jana alisema kuwa pamoja na kufanya vema majaribio yake amekwama kunyakuliwa na timu hiyo kutokana na kuwepo kwa nafasi mmoja tu ya mchezaji aliyehitajiwa na klabu hiyo.
Pazi, alisema mchezaji aliyemzidi kete ni mshambuliaji kutoka nchini Mzimbabwe, ambaye walikuwa wakifanyiwa majaribio kwa pamoja nchini humo.
"Kaka nimerejea usiku wa kuamkia leo baada ya majaribuo yangu ya siku 10 ambapo bahati haikuwa kwangu baada ya Mzimbabwe kunizidi kete kwa sababu nafasi iliyokuwa inawania kuwa moja," alisema Pazi.
Mtoto huyo wa kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Idd Pazi 'Father' alisema pamoja na ndoto zake za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kukwama, hajakata tamaa kutokana na kumwagiwa sifa na kocha mkuu watimu hiyo, Clinton Larsen aliyevutiwa naye.
"Sijakata tamaa kwa sababu nashukuru sikuharibu katika majaribio yangu, tatizo nafasi ilikuwa moja na alihitajika mshambuliaji wakati mie nilienda kule kama winga, na kocha wa klabu hiyo alionekana kuvutiwa nami hivyo nadhani safari bado ipo," alisema Pazi.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kujaribiwa katika klabu iliyowahi kutamba kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani, Kaiserlauten, alisema kurejea kwake kunamfanya aungane na kikosi cha wana JKT kuendelea na Ligi ya nyumbani ambako kesho timu hiyo itaivaa Simba.

Mwisho

No comments:

Post a Comment