STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 6, 2015

Simba wanacheka, walipa kisasi kwa Kagera, Mtibwa hoi

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/HMB_8444.jpg
Simba katika moja ya mechi zao za Ligi Kuu msimu huu
http://kabumbu.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/KIKOSI-SIMBA-SC.jpg
WANAUMEEEE!
SIMBA wanachekaaaa! Baada ya jioni hii kupata ushindi wa mabao 2-1 mbele ya timu ngumu ya
Kagera Sugar katika mechi ya kiporo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Simba ambayo inaendelea kuomboleza vifo vya wanachama wake wa tawi la Maendeleo maarufu
kama Simba Ukawa waliofariki kwa ajali ya gari mjini Morogoro wakati wakielekea Shinyanga
kuwahi pambano hilo pamoja na kifo cha baba wa nahodha wao msaidizi, Jonas Mkude imepumua.
Ushindi huo wa mjini Shinyanga licha ya kusaidia kulipa kisasi kwa wapinzani wao, lakini pia
imewafanya wapunguze pengo la pointi dhidi ya mabingwa watetezi Azam wanashika nafasi ya
pili.
Simba imefikisha pointi 35, moja pungufu na ilizonazo Azam ambao keshokutwa watashuka dimba
la Taifa kuvaana na Wagonga Nyundo wa Mbeya City katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mabao ya washindi katika pambano hilo lililoahirishwa toka Jumamosi kutokana na uwanja wa
Kambarage kujaa maji ya mvua, yaliwekwa kimiani na Ramadhani Singano 'Messi' katika dakika ya
49 kwa shuti kali la mbali na panalti ya Ibrahim Ajibu katika dakika ya 65.
Penalti hiyo ilikuja baada ya mabeki wa Kagera kunawa mpira langoni mwao katika harakati za
kuokoa goli na Ajibu kufunga kiufundi. Kabla ya hapo Rashid Mandawa alifunga bao lake la 10
msimu huu na kumkamata Didier Kavumbagu pale aliposawazisha bao la Messi dakika ya 60.
Katika mechi ya kiporo kingine mapema leo asubuhi Mtibwa Sugar walishindwa kuhimili vishindo vya Stand United na kukubali kichapo cha bao 1-0, kikiwa ni kipigo cha pili kwao mjini Shinyanga.
Awali wiki iliyopita walicharazwa mabao 2-1 na Kagera Sugar na kwa kichapo hicho wameifanya timu hiyo waliokuwa wakiongoza Ligi kwa muda mrefu kuporomoka hadi nafasi ya 12. Nafasi moja juu ya mstari wa timu mbili za kushuka daraja msimu huu kwenda Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
 

Msimamo baada ya matokeo ya  leo ni kama ufuatavyo;

                        P   W   D     L     F      A    Pts
1. Yanga          19   12   4    3    28    11    40
2. Azam FC      18   10   6    2    25    12    36
3. Simba         21    9    8    4    27    15    35
4. Kagera        21    7    7    7    19    20    28
5. Mgambo      20    8    3    9    17    19    27
6. Ruvu           19    6    8    5    13    16    26
7.Coastal         21    5    9    7    14    15    24
8. Mbeya City   20    5    9    6    15    17    24
9. JKT Ruvu     21    6    6    9    16    20    24
10. Ndanda      21    6    6    9    18    24    24
11. Stand         20    6    6    8    15    23    24
12. Mtibwa       21    5    8    7    19    20    23
13. Polisi Moro  21    4    9    8    13    21    21
14. Prisons       19    3    11   5    14    20    20

Mechi zijazo:
KESHO JUMATANO
Azam vs Mbeya CityNo comments:

Post a Comment