STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 6, 2015

YANGA KWELI WANAUMEEEEEEE!

http://3.bp.blogspot.com/-rwwM0C-aX54/VNeMeNEcbvI/AAAAAAABS-s/a7HSjWSMsDg/s1600/DSC_0067.JPGYANGA kweli wanaume! Ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliosalia kwenye michuano ya kimataifa kwa mwaka huu baada ya Azam, KMKM na Polisi Zanzibar kung'olewa mapema. Pia ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki iliyosalia kwenye michuano ya kimataifa, kadhalika ni moja ya klabu tatu pekee za ukanda wa CECAFA zilizopenya katika raundi ya pili ya michuano ya Afrika 2015.
Kwa mujibu wa matokeo ya mwishoni mwa wiki kwa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, Yanga ni timu pekee ya Afrika Mashariki na Kati kusalia katika Kombe la Shirikisho, lakini ikiungana na klabu za Al Merreikh na Al Hilal za Sudan zilizopenya raundi hiyo kupitia Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Yanga ilipata nafasi hiyo ya kuvuka hatua hiyo na kukabiliwa na kibarua kigumu mbele ya Watunisia wa Etoile du Sahel baada ya kuing'oa FC Platinum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 5-2. Mwishoni mwa wiki walitandikwa bao 1-0, lakini ushindi mnono wa mabao 5-1 katika mechi ya awali umewabeba.
Kwa mujibu wa 16 Bora iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu zilizopenya raundi ya pili katika Kombe la Shirikisho ni; Onze Créateurs ya Mali, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Djoliba ya Mali,  Hearts of Oak ya Ghana, ASO Chief ya Algeria, Club Africain ya Tunisia, Warri Wolves ya Nigeria MK Etancheite wa DR Congo, Zamalek ya Misri na FUS Rabat ya Morocco.
Nyingine ni CF Mounana ya Gabon, Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Yanga ya Tanzania, Etoile du Sahel ya Tunia, Royal Leopards ya Swaziland na AS Vita ya DR Congo.
Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika, zipo timu za USM Alger ya Algeria, AS Kaloum ya Guinea,
SM Sanga Balende ya DR Congo,  Al-Hilal ya Sudan, Al-Merreikh ya Sudan, Espérance de Tunis ya Tunisia, MC El Eulma ya Algeria, CS Sfaxien ya Tunisia, AC Léopards ya Congo na Smouha ya Misri.
Klabu nyingine ni Moghreb Tétouan ya Morocco, Al-Ahly ya Misri, Raja Casablanca ya Morocco, watetezi ES Sétif ya Algeria, Stade Malien ya Mali na TP Mazembe ya DR Congo.
Mechi za awali ya hatua hizo zitachezwa kati ya Aprili 17-19 na marudiano kufanyika Mei 1-3 na timu ambazo zitapenya katika Kombe la Shirikisho zitaumana na zile zitakazoangushwa katika Ligi ya Mabingwa kwa ajili ya kuwania kutinga hatua ya makundi kuanza safari ya kusaka mamilioni ya CAF.

No comments:

Post a Comment