STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 5, 2015

NI YANGA NA WATUNISIA, TP MAZEMBE YAPENYA


YAMETIMIA! Wawakilishi pekee wa Tanzania Yanga imefahamika sasa kukutana na Etoile du Sahel ya Tunisia baada ya waarabu hao kulazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Benfica de Luanda ya Angola katika mechi yao ya marudiano ya Kombe la Shirikisho.
Etoile imesonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya mchezo wa kwanza nyumbani kushinda bao 1-0 na sasa watavaana na Yanga waliosonga mbele dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe ambao jana waliwacharaza bao 1-0.
Kipigo hicho cha ugenini hakikuizuia Yanga kusonga mbele kwani ilikuwa na hazina ya ushindi wa mabao 5-1 yaliyopatikana katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.
Mechi ya mkondo wa kwanza ya Yanga na Etoile itachezwa kati ya April 17-19 jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana mjini Tunisia wiki mbili baadaye ambapo mshindi atasubiri kucheza mchujo wa mwisho dhidi ya timu zitakazoangukia pua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye Juni tayari kwa ajili ya kutinga hatua ya makundi kuvuna mamilioni ya CAF.
Aidha TP Mazembe ya DRC imesonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuitoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya leo kushinda nyumbani 3-1 na kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 ugenini.

No comments:

Post a Comment