STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 28, 2014

Alexis Sanchez amkuna Wenger Arsenal

http://pbs.twimg.com/media/BuDK8W3IIAAy0Qv.jpgKIWANGO alichokionyesha mshambuliaji Alexis Sanchez kimemkuna Kocha wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger.
Meneja huyo wa Ze Gunners amesema kiwango cha Alexis Sanchez alichoonyesha katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Besiktas imeinyesha kuwa ana ubora wa kumfanya afanikiwe katika Ligi Kuu nchini Uingereza.
Nyota huo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 35 akitokea Barcelona alifunga bao pekee katika mchezo huo na kuipa Arsenal ushindi mwembamba wa 1-0 katika Uwanja wa Emirates na kuwafanya kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Akihojiwa Wenger amesema Sanchez alionyesha mchezo mzuri kwani alikuwa akielewana vyema na wenzake na alikuwa akionyesha ari ya kupambana huku akiwa hatari anapokuwa katika lango la adui. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ubora huo ndio unaotakiwa katika ligi. Bao hilo la kwanza kwa mchezaji huyo toka ajiunge na timu hiyo alilifunga muda mchache kabla ya mapumziko na kuingiza Arsenal katika ratiba ya makundi yaliyopangwa leo.
Hata hivyo Wenger amekiri kuwa aliingiwa na woga kidogo wakati beki wake Mathieu Debuchy alipotolewa nje kwa baada ya kupewa kadi ya pili ya njano zikiwa zimebaki dakika 14 mpira kumalizika.

No comments:

Post a Comment