STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 10, 2012

TFF YAMPA 'SHAVU' RIDHIWANI KIKWETE

Ridhiwani Kikwete
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania limeteua wadau 10 kwa ajili ya kusaidia timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys itakayopambana na Congo (Brazaville) katika mechi ya raundi ya tatu ya michuano ya awali ya Mataifa ya Afrika.Uteuzi huo umefanywa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga baada ya Kamati ya Vijana ya TFF kufanya kikao chake kujadili kwa umakini ushiriki wa timu hiyo na kupeleka mapendekezo yake kwa rais huyo wa shirikisho.
Kutokana na umuhimu wa mechi hiyo itakayoamua timu itakayofuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, TFF imeona umuhimu wa kuwa na kamati ambayo itakuwa na majukumu mawili makubwa ambayo ni:

1. Kuhamasisha vijana waone umuhimu na kuwa na ari ya kushinda mechi hiyo

2. Kuhamasisha umma uone umuhimu wa mechi hiyo na hivyo kuisaidia iweze kufuzu.

Walioteuliwa kuunda kamati hiyo ni:
1. Ridhiwani Kikwete                                    Mwenyekiti
2. Ahmed Seif (Magari)                                 Mjumbe
3. Nassoro Bin Slum                                      Mjumbe
4. Henry Tandau                                            Katibu
5. Ahmed Mgoyi                                            Mjumbe
6. Aboubakar Bakhresa                                 Mjumbe
7. Angetile Osiah                                           Mjumbe
8. Kassim Dewji                                             Mjumbe
9. Abdallah Bin Kleb                                     Mjumbe
10. Salim Said                                                Mjumbe

Baada ya kuvuka raundi mbili za kwanza bila ya kucheza mechi kutokana na wapinzani wake kujitoa, timu ya Serengeti Boys inahitaji kufanya kila iwezalo kuweza kuiondoa Congo kwenye mashindano hayo na kuweka rekodi ya kufuzu kucheza fainali hizo za Afrika ambazo pia zitatoa wawakilishi wa Afrika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.

Mechi za kwanza za raundi ya tatu zitachezwa kati ya Novemba 16 na 18, 2012 na mechi za marudiano zitachezwa kuanzia Novemba 30, 2012 hadi Desemba 2, 2012.


No comments:

Post a Comment