STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 21, 2013

Ile Ile atoa Wazazi akijipanga upya

Msani Ile Ile katika pozi
MSANII anayekuja juu kwenye muziki wa kizazi kipya, Maishani Ndee 'Ile Ile' ameachia kibao kipya kiitwacho 'Wazazi' ukiwa ni wimbo wake wa tatu tangu atumbukie kwenye fani hiyo miaka minne iliyopita.
Wimbo huo na video yake umeanza kuwa gumzo kwenye vituo vya redio na runinga kutokana na maudhui wake na Ile Ile alisema amefarijika na anajipanga kuandaa kazi nyinginje mbili kwa mpigo.
Ile Ile aliyewahi kukimbiza na nyimbo za 'Ileile' alioutoa mwaka 2010 na 'Bora Twende' wa mwaka jana alisema nyimbo ambazo zitafuata baada ya 'Wazazi' ni 'Amani na Upendo' na 'Sheila'.
"Hizi zimeshakamilika kila kitu na wakati wowote naziingiza studio kuzirekodi ili kuendelea kuwapa burudani mashabiki wangu na muziki kwa ujumla," alisema Ileile anayejishughulisha na biashara za nguo na hasa lebo yake ya Ile Ile Wears.
Msanii huyo mwenyeji wa Kondoa, alisema angetamani kutoa albamu yake ya kwanza, lakini soko la muziki kwa sasa nchini linamtisha na hivyo anaona bora aendelee kurtoa 'singo' moja moja na video zake ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kupata shoo zitakazomuingiza pato la kutosha.

No comments:

Post a Comment