STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, June 25, 2013

After Death ya Kanumba kuachiwa hadharani Julai 30

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEis_FnvkJ3vrjIRirZl9Qxb0BdfdsIQOCGQIcqOV2__0kfCDRjnU1KnQlIoCR3nyI5i-BS2k8HEbNq1Vcn_QcZlXS3S5qzbXof7eyCdW71O0Q0WyQVcEVz5ILvAToRDjFipfsZ9UUF30TI/s1600/Kanumba1.jpeg

FILAMU iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo 'After Death' na iliyozinduliwa rasmi katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu msanii huyo aage dunia inatarajiwa kuachiwa mtaani mwezi ujao.
Filamu hiyo iliyotungwa na tayarishwa na msanii Jacklyne Wolper na kuongozwa na Leah Richard 'Lamata' ilipangwa kutolewa mwezi huu wa Juni, lakini Lamata aliiambia MICHARAZO kwamba kazi hiyo itaachiwa rasmi Julai 30 mwaka huu.
Lamata alisema wameamua kusogeza muda wa kuiingiza sokoni kutokana na foleni kubwa iliyopo kwa wasambazaji na pia kujipanga kuweza kuwafikia mashabiki karibu wote nchini, ikiwa ni siku chache baada ya kuiachia hadharani filamu ya "my Princess'.
"Baada ya kuachia 'My Princess' tunajipanga kuitoa hadharani 'After Death' filamu maalum iliyotengenezwa kwa ajili ya kumuenzi Kanumba, tumepanga kuiachia Julai 30," alisema Lamara.
Ndani ya filamu hiyo imeshirikisha wasanii chipukizi walioibuliwa na marehemu Kanumba kama Patrick na Jennifer, wamo pia Branco, Uncle D, Shamsa Ford, Wolper, Mainda, Patcho Mwamba, Stanley Msungu na wengine ambao walikuwa wakiigiza na msanii huyo.
Kanumba alifariki Aprili 7 mwaka jana baada ya kuanguka katika kilichoelezwa ugomvi baina yake na mpenzi wake, Elizabeth Michael 'Lulu'  na kuacha majonzi kwa mashabiki na wale waliokuwa wakifanya naye kazi kutokana na ufanisi wake katika tasnia ya filamu na uigizaji kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment