STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 2, 2014

Dani Alves amtetea Neymar Barca

BEKI wa Barcelona, Dani Alves amemtetea Mbrazil mwenzake Neymar anayeshutumiwa kwa kushindwa kucheza kulingana na kiasi kikubwa cha pesa kilichotumika kumnunua kutoka katika klabu ya Santos ya Brazil.
Kabla ya mechi ya jana usiku dhidi ya Atletico Madrid, Neymar alikuwa amefunga magoli matatu tu na kutoa pasi moja ya goli katika mechi tisa alizokuwa amecheza baada ya kurejea akitokea kuwa majeruhi na alikosa nafasi tatu za wazi za kufunga katika mechi waliyoshinda 1-0 dhidi ya Espanyol Jumamosi.
"Nadhani shutuma dhidi yake zilianza baada ya dondoo za mkataba wake zilipotoka, kabla ya hapo kila mtu alikuwa na furaha naye. Hatupaswi kumhukumu kwa kuangalia ni kiasi gani aligharimu, bali tuangalie ni vizuri kiasi gani anacheza.
"Kwa mtazamo wangu mimi anacheza vizuri kama alivyoanza mwanzo wa msimu. Na daima ni lazima utarajie apate muda wa kuizoea ligi kwasababu amehamia katika nchi mpya, lakini anacheza vizuri," alisema Alves.

No comments:

Post a Comment