STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 2, 2014

Ni Real Madrid au Dortmund kucheka Ulaya, Chelsea waifuata PSG


REAL Madrid leo watakuwa nyumbani kuwakabilia wanafainali wa mwaka jana wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Borussia Dortmund katika mchezo wa roibo fainali ya michuano ya mwaka huu, huku Chelsea watakuwa ugenini kuwakabili PSG katika mchezo miwngine mkali.
Reala Madrid iliyozinduka hivi karfibuni baada ya kubamizwa mechi mbili mfululizo katika ligi ya nchini mwao na kujikuta wakiporomoka toka kileleni mwa msimamo hadi nafasi ya tatu watakuwa na kazi kubwa ya kuwazuia Wajerumani wasiwaletee madhara kwenye uwanja wao wa Santiago Bernabeu.
Hata hivyo kocha mkuu wa timu hiyo, Carlo Ancelotti ametamba kwamba anajivunia kuwa na timu kabambe alizowahi kuzinoa na kuamini kwamba wataifumua  Dortmund leo.
MUitalia huyo alisema kuwa anajivunia kuwa na wachezaji nyota ambao wameifanya timu hiyo kuwa katika nafasi znuri ya kunyakua mataji matatu kwa msimu huu.
“Mbali na mabingwa kama Cristiano Ronaldo, ninao wachezaji wengi wazuri makinda pamoja na wazoefu. Ninataka kuonyesha ukweli kuwa msimu huu si [Gareth] Bale tu aliyetua hapa, lakini pia wachezaji watano kutoka kikosi cha makinda.”
Madrid bado ipo katika nafasi ya kutwaa makombe matatu msimu huu, kwani vijana wa Ancelotti kwa sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye La Liga, wakati wakiwa na mchezo wa fainali wa Kombe la Mfalme (Copa del Rey) dhidi ya Barcelona wakiwa pia kwenye kinyang'anyiro cha Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya  Dortmund.
Hata hivyo kocha huyo wa 'Blancos' amesisitiza kuwa lengo kubwa la klabu hiyo msimu huu ni kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10.
“Ndoto za Real Madrid kwa sasa ni kutwa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya,” Ancelotti alisema.
Katika mechi nyingine ya robo fainali, wenyeji PSG kupitia kocha wao,  Laurent Blanc wamedai wanaihofia Chelsea kwa uimara wa ukuta wao..
Mabingwa hao wa Ligue 1, wameshinda mechi zote nane za michuano hiyo lakini beki wa kati wa zamani wa Ufaransa, Blanc anajua vema kuwa Chelsea,  chini ya Jose Mourinho, ina uzoefu na safu ya ulinzi imara ya kuweza kukabiliana na wapinzani wowote.
"Tutapaswa kuwa makini zaidi," alisema Blanc. "Tutakuwa na nafasi chache na tutakazozipata itabidi kuzitumia. Tunajua tunapaswa kuwa katika daraja lingine.
PSG ilisonga mbele bila kupoteza katika kundi lililozozijumuisha Anderlecht, Porto na Olympiakos Piraeus kabla ya hatua ya mtoano ya 16 bora kuitupa nje Bayer Leverkusen.
Tegemeo kubwa katika mechi hiyo kwa Blanc litakuwa ni mshambuliaji wake anayeona nyavu zaidi, Zlatan Ibrahimovic ambaye msimu huu wa Ligue 1 ameshatupia mabao 25, yakiwa ni 11 zaidi ya wanaomfuatia, mchezaji mwenza  Edinson Cavani na Alexandre Lacazette wa Olympique Lyon.
Ibrahimovic pia ameshafunga mabao 10 msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa mara ya mwisho Chelsea kucheza Uwanja wa Parc des Princes ilikuwa 2004-05 kwenye hatua ya makundi, ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Mourinho kuiongoza klabu hiyo ya London katika michuano ya Ulaya ambapo waliichapa PSG 3-0.
Mourinho leo atashusha kikosi chake uwanjani akiwa na kumbukumbu mbaya ya kipigo cha bao 1-0 alichokipata Jumamosi kwenye Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace.

No comments:

Post a Comment