STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 2, 2014

Ngoma ya Dar Modern yapasuka videoni

Hassan Vocha
KUNDI la muziki wa taarab la Dar Modern 'Wana wa Jiji', limeiachia hadharani video ya albamu yao ya 'Ngoma Imepasuka' ambayo ni kati ya albamu zao mbili mpya walizozizindua wakati wa Siku ya Wapendanao.
Albamu yao nyingine ni 'Ooh My Honey' ambayo nayo imesharekodiwa video yake, lakini uongozi wa kundi hilo umeamua kuachia moja ili watu wapate uhondo kwa awamu.
Akizungumza na MICHARAZO, mmoja wa waimbaji wa Dar Modern, Hassan Kumbi 'Hassan Vocha' alisema video hizo mbili zililzokuwa zikirekodiwa Lushoto Tanga, zimekamilika na imeachiwa moja, huku nyingine ikiwekwa 'mafichoni' kwanza.
"Tunashukuru tumemaliza kurekodi vodeo za albamu zetu mbili na tumeachia moja ya 'Ngoma Imepasuka' ambayo imeanza kurushwa hewani tangu mwishoni mwa wiki ikiwa na nyimbo sita," alisema Hassan Vocha.
Muimbaji huyo mpya wa kundi hilo aliyeibuliwa na Kituo cha Mkubwa na Wanae, alizitaja nyimbo zilizopo kwenye video hiyo ni 'Ngoma Imepasuka' yenyewe, 'Siwanyimi Uzuri', 'Nakwendakwa Mume Wangu' na 'Sikuamini Macho Yangu'.
"Video ya pili pia ina nyimbo sita, ila imepangwa kuachiwa baadaye mwezi ujao," alisema Vocha aliyepata jina hilo kutokana na wimbo wake wa 'Vocha' alioimba na katika mduara na Dogo Aslay wakati akiwa Mkubwa na Wanae kupata umaarufu mkubwa.

No comments:

Post a Comment