STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 1, 2014

Droo Play-offs Kombe la Shirikisho yatoka

Al Ahly iliyoangushiwa Wamorocco, watavuna nini?

DROO ya mchujo wa kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, liemtangazwa leo mjini Cairo, ambapo waliokuwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri imeangukia mikononi mwa Difaa Hassani Jadida ya Morocco.
Al Ahly itakutana na Wamorocco hao wakiwa na kumbukumbu ya kuvuliwa taji la Afrika na Waarabu wenzao wengine wa Libya mwishoni mwa wiki.
Ratiba hiyo pia imeziingiza mbili za Mali, AS Real na Djoliba zimepangwa pamoja katika mechi hizo. Ratiba hiyo ya upangaji wa droo leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri na kuongozwa na Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El-Amrani aliyesaidiwa na Hazem El-Hawary, Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya shirikisho hilo. Timu zilizotolewa katika Hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika zimepangwa na timu zilizofuzu Nane Bora ya Kombe la Shirikisho.
AS Real, waliofungwa katika Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1966 watamenyana na wapinzani wao wa jadi, Djoliba, waliofungwa kwenye ya Kombe la Shirikisho miaka miwili iliyopita kuwania kuingia Hatua ya makundi.
Medeama ya Ghana itamenyana na mabingwa wa mwaka 2012, AC Leopards ya Kongo wakati Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini itamenyana na vigogo wa Ivory Coast, ASEC Mimosas.
Mabingwa wa Cameroon, Coton Sport watamenyana na Petro Atletico ya Angola wakati Etoile du Sahel ya Tunisia itamenyana na Horoya ya Guinea.
Bayelsa United ya Nigeria itamenyana na Sewe Sport ya Ivory Coast katika pambano la timu za Magharibi mwa Afrika tupu, wakati Nkana ya Zambia itamenyana na Club Athletique Bizertin ya Tunisia.

Ratiba kamili ya mchujo huo kuwania kutinga hatua ya makundi ni kama ifuatavyo:
Al-Ahly (Misri) vs Difaa Hassani Jadida (Morocco)
AS Real (Mali) vs Djoliba (Mali)
AC Leopards (Kongo) vs Medeama (Ghana)
Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) vs ASEC Mimosas (Ivory Coast) 
Coton Sport (Cameroon) vs Petro Atletico (Angola)
Horoya (Guinea) vs Etoile du Sahel (Tunisia)
Sewe Sport (Ivory Coast) vs Bayelsa (Nigeria)
Nkana (Zambia) vs Club Athletique Bizertin (Tunisia)
(Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Aprili 18, 19 na 20 wakati marudiano itakuwa kati ya Aprili 25, 26 na 27,mwaka 2014

No comments:

Post a Comment