AFC Arusha miongoni mabingwa wa mikoa ambao majina yao yamewasilishwa TFF |
Mabingwa hao ni Arusha (AFC), Kilimanjaro (Panone FC), Lindi (Kariakoo SC), Manyara (Tanzanite SC), Mara (JKT Rwamukoma), Morogoro (Volcano FC), Mtwara (Pachoto Shooting Stars), Pwani (Kiluvya United), Shinyanga (Bulyanhulu FC), Singida (Singida United) na Tanga (African Sports).
Mikoa ambayo haijawasilisha mabingwa wake ni Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Katavi, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Simiyu na Tabora wakati mikoa ya Dodoma na Mwanza imeomba kuongezewa muda kutokana na sababu mbalimbali.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliagiza kuwa mikoa yote iwe imemaliza ligi na kuwasilisha jina la bingwa wake Machi 30 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment