KIKOSI
cha watu 27 wakiwemo wachezaji na benchi la ufundi cha timu ya Taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kinatarajia
kuondoka keshokutwa (Aprili 3 mwaka huu) kwenda Nairobi, Kenya.
Ngorongoro
Heroes inayofundishwa na John Simkoko ipo kambini tangu Machi 23 mwaka
huu kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya (U20). Mechi hiyo ya michuano ya
Afrika kwa vijana wenye umri huo itachezwa Jumapili (Aprili 6 mwaka huu)
saa 10 kamili jioni Uwanja wa Machakos ulioko kilometa 80 kutoka jijini
Nairobi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo (Aprili 1 mwaka huu), Kocha
Simkoko amesema wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, na
nia ni kupata matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa
nchini wiki tatu baadaye.
Kikosi
cha Ngorongoro Heroes chenye wachezaji 20 na viongozi saba kitaondoka
saa 4.30 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways. Msafara wa timu hiyo
utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Mpira wa Miguu wa Vijana.
Mechi
hiyo itachezeshwa na waamuzi Abdoulkarim Twagiramukiza, Ambroise
Hakizimana, Raymond Bwiliza na Louis Hakizimana wote kutoka Rwanda
wakati Kamishna ni Maxwell Mtonga wa Malawi.
Ngorongoro Heroes itaagwa kesho (Aprili 2 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF.
No comments:
Post a Comment