STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 12, 2014

Miyeyusho, Cheka kuvuna nini leo PTA?

Miyeyusho (kulia) na mpinzani wake walipopima uzito jana

Cheka akipimwa uzito huku mpinzani wake kutoka Iran akishuhudia
MABONDIA  Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ na Francis Cheka 'SMG' wanatarajiwa kupanda ulingoni leo kwenye ukumbi wa PTA, Dar es Salaam kupambana na wageni kutoka Thailand na Iran.
Miyeyusho atazipoga na Sukkasem Kietyongyuth na Cheka akivaana na Gavad Zohrehvand kutoka Iran katikkaa mipambano isiyokuwa na ubingwa.
Pambano hilo la Miyeyusho litakuwa la raundi 10 na linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na mabondia wote kujiandaa vizuri.
“Maandalizi niliyofanya ni makubwa, hii yote kwa sababu sitaki kuwaangusha Watanzania, kwani hili ndilo pambano langu la kwanza la kimataifa kufanyika katika ardhi ya nyumbani, hakuna haja ya kupoteza zaidi ya ushindi wa K.O,” alisema Miyeyusho. 
Pambano la Cheka litakuwa la raundi nane na litakuwa la utangulizi. 
Promota wa pambano hilo, Mussa Kova, amewataka wapenzi wa mchezo huo kujitokeza kwenye mapambano hayo ya kihistoria.
Cheka atapanda ulingoni ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipotwanga Urusi na kupoteza taji lake la Dunia la WBF alilolitwaa Agosti 30 kwa kumpiga Mmarekani, Phil Williams.
Katika michezo hiyo pia kutakuwa na mechi za utangulizi zitakazowakutanisha mabondia mbalimbali za jijini Dar es Salaam likiwa kati ya Ibrahim Class dhidi ya Mustafa Dotto.

No comments:

Post a Comment