STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 14, 2014

WENGER HAJUTII KUTOMSAJILI FABREGAS

http://static.sportskeeda.com/wp-content/uploads/2014/06/104741_heroa-1402851267.jpgKOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesisitiza kwamba hajuti kumsajili Cesc Fabregas katika kipindi kilichopita cha usajili.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alijiunga na Chelsea akitokea Barcelona kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 27 mwezi Juni na ametisha chini ya Mourinho akitoa pasi za mwisho zilizozaa magoli 7 katika mechi 7, idadi ambayo ni sawa na pasi za mwisho zote zilizopigwa na timu nzima ya Arsenal hadi sasa.
Fabregas ambaye aliichezea Arsenal kwa miaka nane kabla ya kurejea Barcelona 2011, alibainisha katika barua yake ya wazi kwamba Arsenal walikataa kukitumia kipengele cha mkataba cha kumsajili tena kama wanamhitaji kabla ya klabu nyingine kupewa ofa hiyo.
Lakini, Wenger amesisitiza kwamba ana wachezaji wengi wa eneo la kiungo na anaamini kwamba timu yake itapunguza pengo la pointi dhidi ya Chelsea licha ya kulala 2-0 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge kabla ya wikiendi ya mechi za kimataifa. 
"Sijutii kutomchukua Cesc kwa sababu tayari tuna wachezaji wengi wa ubunifu katika eneo letu la kiungo," Wenger aliiambia BeIN Sports.
"Chelsea watatakuwa na kipindi kigumu (katika msimu). Ratiba yetu ilikuwa ngumu mno na ninaamini kwamba tunaweza kuziba pengo dhidi yao."

No comments:

Post a Comment