STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 14, 2013


SIMBA, AZAM HAKUNA MBABE, YANGA YAPUMUA KILELENI

 Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa akichuana na beki wa Azam FC, John David katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilifunga mabao 2-2 (Picha na Habari Mseto Blog)  
 Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Azam FC, Joockins Atudo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu  Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
 Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kuapata bao la pili.
Kiungo wa timu ya Simba, Abdallah Seseme akiwatoka wachezaji wa Azam FC, Himid Mao (kulia) na Salum Abubakar wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2.

LICHA ya tambo nyingi kabla ya pambano lao timu za Simba na Azam jioni ya leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na kuwafanya vinawa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kupumua.
Yanga mabo mashabiki wake leo walionyesha kioja kwa kuwashangilia watani zao Simba dhidi ya Azam, wanapumua kwa vile Azam inayowafukuza kwenye mbio za ubingwa imepunguza pengo la pointi moja tu na kuipa nafasi Yanga kuhitaji pointi tano tu kati ya mechi zake nne zilizosalia kutangaza ubingwa msimu huu.
Yanga yenyewe ina pointi 52 wakati Azam waliopo nafasi ya pili wana pointi 47, huku kjwa sare hiyo ya leo Simba imeendelea kusalia kwenye nafasi ya nne akiwa na pointi 36.
Ramadhani Singano 'Messi' ndiye aliyeipa Simba uongozi wa mabao katika pambano hilo lililochezeshwa na mwamuzi Oden Mbaga kwa kufunga mabao mawili katika dakika ya 10 na 14 akimalizia kazi murua iliyofanywa kwa ushirikiano wa Mrisho Ngassa na Haruna Changono.
Dakika ya 29 Kipre Tchetche aliifungia Azam bao la kwanza baada ya Khamis Mcha kuangushwa akielekea kumsalimia kipa Abel Dhaira na kumfanya afikishe bao la 15 msimu huu.
Dakika mbili baadaye kocha wa Azam, Stewart Hall alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kutokana na maamuzi yake na hadi mapumziko matokeo yalikuwa mabo 2-1.
Kipindi cha pili Azam walionyesha uhai zaidi kwa kushambulia lango la Simba na kufanikiwa kupata bao la pili na la kusawazisha dakika ya 72 kupitia kwa Humphrey Mieno.
Kwa matokeo ya pambano hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kutokana na tambo zilizokuwa zikitolewa na pande zote mbili na mkasa ulioibuka baada ya mechi yao ya kwanza ambapo Simba walishinda mabao 3-1 na kupelekea Azam kusimamisha wachezaji wake wanne kwa tuhuma za rushwa, msimamo upo hivi;


                                       P     W     D     L     F     A     D     PTS
    1.  Young Africans       22    16     4     2    40    12    28    52
    2. Azam                      23    14     5     4    41    19    22    47    
    3 . Kagera Sugar         22    10     7     5    25    18    7      37     
    4.  Simba                     22     9     9     4     32    21    11    36
    5.  Mtibwa Sugar         23     8     9     6     26    24     2     33   
    6. Coastal Union          22     8     8     6     23    20     3     32    
    7.  Ruvu Shooting         23     8     6     9     21    22    -1    30     
    8.  JKT Oljoro FC       23     7     7     9     22     27    -5    28     
    9. Tanzania Prisons       24     6     8    10    14     21    -7    26    
    10.JKT Mgambo         22     7     3     12    14     22    -8    24
    11.Ruvu Stars              21     6     4     11     19     34   -15   22
    12. Toto Africans         24     4    10    10     22     32   -10   22
    13. Polisi Morogoro     23     3    10    10     11     21    -10  19    
    14.  African Lyon         23     5     4     14     16     35    -19  19

No comments:

Post a Comment