STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 3, 2014

Nahodha Ngorongoro ahidi ushindi Kenya

http://1.bp.blogspot.com/-vnFsbMFfWIE/Ug-jLjmJ7sI/AAAAAAAAxew/QkAT-OhkRQM/s1600/IMG_0938.JPG
Aishi Manula akiwajibika uwanjani na timu yake ya Azam
NAHODHA wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Aishi Manula amesema wamejipanga kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mechi dhidi ya Kenya itakayochezwa Jumapili (Aprili 6 mwaka huu) katika mji wa Machakos.
Akizungumza jana (Aprili 2 mwaka huu) kwenye hafla ya kukabidhiwa bendera kwa timu hiyo kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Manula ambaye pia anaidakia timu ya Azam alisema lengo lao ni kufanya vizuri kwenye mechi hiyo.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda akikabidhi bendera hiyo, aliwataka wachezaji hao kujituma na kutanguliza uzalendo mbele bila kusahau kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni ushirikiano.
Alisema Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, hivyo waliopata fursa ya kuwemo Ngorongoro Heroes wakati huu wajue kuwa wamepata bahati, na wanatakiwa kufahamu kuwa wao ni wawakilishi wa Tanzania, na Watanzania wana kiu ya kusikia matokeo ya mechi hiyo.
Ngorongoro Heroes inayofundishwa na John Simkoko inaondoka kesho (Aprili 3 mwaka huu) saa 4.30 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways, na mara baada ya kuwasili itakwenda moja kwa moja kwenye hoteli ya Garden iliyopo Machakos ambayo ndiyo imepangiwa kufikia na Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF).
Wachezaji waliopo kwenye msafara huo unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF), Ayoub Nyenzi ni Abrahman Mohamed, Aishi Manula, Ally Idd, Ally Mwale, Athanas Mdamu, Ayoub Semtawa, Bryson Raphael na Edward Manyama.
Wengine ni Gadiel Michael, Hamad Juma, Hassan Mbande, Ibrahim Ahmada, Idd Ally, Kelvin Friday, Michael Mpesa, Mohamed Ibrahim, Mudhathir Yahya, Pato Ngonyani, Peter Manyika na Salum Mineli.

No comments:

Post a Comment