STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 18, 2015

Rais Kikwete apangua Ma-DC, Mwakalebela, Kisu waula!

https://pamelamollel.files.wordpress.com/2013/02/frederick-mwakalebela.jpg
Mwakalebela

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/12/kiss.jpg
Shaaban Kissu (kulia)

Na Rahim Junior, Dodoma 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete ameendelea kufanya panga pangua katika serikali yake baada ya kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Ma-DC wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya awali.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, leo mchana, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais  Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.
Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni; Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilaya ya Wanging’ombe.
Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Mtangazaji wa TBC, Shaaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).
Waliotenguliwa uteuzi wao lakini watapangiwa majukumu mengine ni'; Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa; ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).

No comments:

Post a Comment