STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 7, 2014

'Wasanii kuweni wabunifu mteke soko la kimataifa'

Vitalis Maembe
WASANII nchini wamekumbushwa kuwa wabunifu zaidi na kuvuka mipaka ya nchi ili kuweza kujitangaza katika anga la kimataifa badala ya kuridhika kutamba nyumbani tu.
Wito huo umetolewa na mwanamuziki mahiri, Vitalis Maembe alipokuwa akizungumza na wasanii wa Kaole Sanaa hivi karibuni ambapo alisema umefika wakati wasanii wakaacha kujiangalia wenyewe kwa wenyewe nchini na badala yake kutupa macho nje na kutoa vitu vitakavyowatangaza wenyewe na taifa kwa ujumla.
Staa huyo wa nyimbo za 'Sumu ya Teja' na 'Kariakoo' alisema soko la kimataifa lina manufaa makubwa kwa wasanii kama wakiamua kulichangamkia na kuwasisitiza wajikite kwenye ubunifu na hasa kulenga vionjo vya Kitanzania kurahisisha utambuzi wa kazi hizo.
"Ubunifu na hasa utakaojikita kwenye vionjo vya Kitanzania ili kujitofautisha na kazi za wengine ni mambo yanayopaswa kuzingatiwa na mimi nipo tayari kuwasaidia yeyote mwenye kuhitaji msaada wangu, ilimradi kusogeza mbele gurudumu la sanaa Tanzania," alisema.
Maembe aliwamwagia sifa kundi la Kaole kwa namna walivyoibua wazo la kurejesha kundi hilo lililoanzisha mwaka 1996 na kutamba na michezo yao mbalimbali kwenye vituo vya ITV na TVT kabla ya kutoweka baada ya nyota wake kujitosa kwenye uigizaji wa filamu.

1 comment:

  1. Itapendeza zaidi kama wasanii wote pamoja na watu wengine kwa ujmla watajiongeza kwa kujitangaza, maana waswahili usema kwamba biashara ni matangazo. kwaiyo niwajibu wa kila mtu kujiongeza kwa kujitangaza, ili aweze kufahamika zaidi.
    http://mutalemwa-masgider.blogspot.com

    ReplyDelete